Dalili za Ugonjwa wa Homa ya INI na Jinsi Unavyoambukizwa ( Ugonjwa huu ni hatari kuliko UKIMWI)
Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivyo vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus).
Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye Kifo.
JINSI UNAVYOAMBUKIZWA:
Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu.
Njia kuu za maambukizi :
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi 'denda'
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki
-kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo
-kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya Ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya Ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
No comments:
Post a Comment