MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com,instagram@mwalim_yuu.Fb.com/
SEHEMU YA 29.
Tulipoishia, Nilipofika na kushika kichwa kiliporomoka na kuanguka chini. Alikua kashakatwa kichwa kwamana ni mfu tayari. Nikiwa nawaza nini nifanye mara ghafla_____Enda nayo....... Nikasikia mlango unagongwa. Nikiwa nimeduwaa najiuliza nifanye waliingia askari wakiwa wameshikilia mitutu ya bunduki kisha wakasema hapohapo ulipi inua mikono juu. Uko chini ya ulinzi. Niliinua mkkono afande mmoja akaja na kunifunga pingu kisha wakaniamuru kutoka nje na kwenda kituoni. Nilitii baada ya kufika kituoni niliingizwa mahabusu na kulala humo usiku ule. Asubuhi nilifuatwa na kuambiwa kesi yangu tayari iko mahakamani na nahitajika kwenda kujibu mashitaka. Nilitolewa nikapandishwa kwenye karandinga kuelekea mahakamani.
Tulifika mahakama ya Kisutu kesi yangu ikawa kesi ya kwanza kusomwa. Nilisomewa mashitaka mawili ambapo moja ilikua ni kuua bila kukusudia, na la pili ni udanganyifu ambapo nilimdanganya mkuu wa kituo kua aje nyumbani kwangu ili tumalize ugomvi wetu na alipofika nikamuua kwa kumchoma visu. Vielelezo vya ushahidi vikaletwa kwanza ni mawasiliano ya simu ambapo ilionekana namba yangu ilikua ikiwasiliana na Marehemu huku nikimshawishi aje nyumbani kwangu tuyamalize. Ushahidi wa pili ni mkanda wa video ambao ulirekodiwa kwa siri mimi nikiwa namuua Mkuu wangu pale nyumbani kwangu. Chaajabu ni kua ni kweli muuaji aliyekua akionekana alikua ni mimi.
Ushahidi wa tatu alikua ni shuhuda aliyenishuhudia kwa macho yake. Kwaamara ya kwanza nikamwona Peris akisimama na kuthibitisha kua mimi ndiye niliyeua na yeye ndiye alinirekodi. Hapakua na mda wa kuuliza Peris alikua wapi na kwanini aliacha kazi ghafla. Hayo yote yalifunikwa mimi tuu ndo nilikua naangaliwa. Maswali kichwqni yalijaa nikiwa najiuliza ni kesi gani hapa Tanzania ilifanyiwa uchunguzi ndani ya usiku mmoja na ushahidi kukamilika? Mbona kesi yangu ilichukua mda mfupi sana. Kuna watu miaka saba hua mahabusu kesi yangu imewezekanaje? Na pili kwanini nihukumiwe kwa kosa la kuua bila kukusudia ikiwa mimi ndiye nilimwita na kumuua. Zaidi nikajiuliza Peris alipiga picha na kuzipeleka polisi je mbona hawakumkamata wakati ni mtuhumiwa.
Maswali yalikua mengi ambayo hata majibu nilikuwa sina. Nilipigwa na butwa uchungu ukanitawala. Nikamlaani Zabroni, nikamlaani Peris, Nikalaani jeshi la polisi kwa kushindwa japo kunitetea hata kidogo. Zaidi wao waliongeza ushahidi wa kuwa nilikuwa na ugomvi na marehemu hivyo nimemuua kwa makusudi. Nililaumu sana machozi yalinitoka bila kikomo afande nilimwaga chozi kizimbani. Kisha nikamsikia hakimu mfawidhi wa mahakana ya Kisutu akiuliza je mshitakiwa una utetezi wowote juu ya haya yote?
Sikua na la kuongea zaidi ya kulia tuu kwa uchungu. Aliuliza tena una utetezi? Nikajibu kwa gadhabu sina utetezi zaidi ya kusema mimi sihusiki. Basi hakimu akasoma hukumu na kusema Ndugu Yusuph Abel Ng'ahala unahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na hukumu hiyo utaanza kuitumikia sasa hivi. Nilishangaa kesi gani ya mauaji ufungwe miaka mitano? Nilijiuliza mambo mengi nadhani kesi yangu iliweka rekodi ya kua kesi pekee iliyochukua mda mfupi kuichunguza na kuitolea hukumu. Hakuna kesi hapa Tanzania iliyowahi kusomwa na kwa mda mfupi kama yangu nadhani kuna namna iliamrishwa nifungwe ili watu wengine waendelee na mambo yao kwa uhuru.
Nililia sana kama mtoto mdogo. Askari walikuja wakanitoa kizimbaniyangu.unipeleka kwenye karandinga. Nikakaa kusubiri wenzangu. Afisa upelelezi nilifungwa pingu kwa kosa ambalo sikulifanya, afisa mzima niliwekwa chini ya ulinzi sasa. Afisa mzima wa upelelezi nikahukumiwa kwa kosa la uuaji. Haki iko wapi Tanzania, haki iko wapi, nani anasimamia haki ikiwa hata mahakama haikuchunguza kwa makini. Je wanyonge twende wapi jamani Nalia na tanzania naipenda Tanzania niliapa kuipigania mpaka nakufa lakini mbona nalipwa nisichostahili. Serikali yangu iko wapi, Sheeia mbona wanazijua wachache nililia sana huku nikitafakari mambo mengi sana.
Nilipambana kila nilipopaswa kulitetea taifa la Tanzania, niliapa kuilinda mpaka kufa nilitamani amani na upendo aliouacha mwalimu Julius kambarage Nyerere udumu miongoni mwetu. Sikupenda watu wachache kama Zabroni waharibu amani yetu. Nilitamani siku moja nione kila mtu anafurahia mema ya Tanzania naipenda nchi yangu. Nilijikuta naimba wimbo wa zamani kidogo huku nalia. Nilitiririka machozi ndani ya karandinga huku nikiimba.
"Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana!
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo woteeeee!!!"
Wakati namaliza kuimba niliwafanya wale maaskari magereza kubaki wameduwaa wakiniangalia na kunishangaa. Niliipenda nchi yangu lakini ni watu wachache wakafanya niwe kama msaliti kwa taifa langu. Kwanini lakini sikuangaliwa mema yangu niliyofanya nikiwa na jeshi la polisi. Kwanini sikuchunguzwa kama wengine. Kwanini sheria haikuangaliwa mara mbili hatimae ikamuhukumu mtu asiye na hatia. Tunaipeleka wapi nchi kwa mwenendo kama huu?
Sikua na jinsi wala lingine la kufanya. Nilimkumbuka mama kijijini ananitegemea. Baba alitegemea uwepo wangu Kaka zangu walikuwa hawana mbele wala nyuma mimi ndo kilikuwa kichwa cha familia na sasa naenda jela. Baba na mama wataishi vipi. Maisha yalibadilika ghafla kutoka kwenye uzuri na kuwa mabaya yasiyofaa hata kidogo. Nilihisi dunia imenitenga. Nililia sana kwakweli sikuona mchango wangu kuthaminiwa na taifa hili. Nikiwa bado nalia kwa uchungu mara kuna wengine watatu wakaongezeka mle kwenye karandinga kisha gari taratibu ikaanza safari kuelekea jela. Huko ndiko tulipaswa kutumikia vifungo vyetu hakika inauma________________________
SEHEMU YA 30.
Tulipoishia, Nikiwa bado nalia kwa uchungu mara kuna wengine watatu wakaongezeka mle kwenye karandinga kisha gari taratibu ikaanza safari kuelekea jela. Huko ndiko tulipaswa kutumikia vifungo vyetu hakika inauma_______Endelea sasa.........Inauma haswaa tena ukiwa siyo mkosaji na sheria ikapindishwa ili tuu kukuona ukiingia jela. Nililia sana lakini kilio changu kilikua kilio cha samaki machozi kwenda na maji. Lakini nilishindwa kujizuia kulia kila nilipogundua kuonewa, kusingiziwa na kutengenezewa matukio na watu wasiopenda amani yetu ya taifa.
Tulifika gereza la Keko, hili gereza lilisifika sana kwa kua na wafungwa wa aina mbalimbali. Pia ni miongoni mwa magereza maarufu sana hapa nchini. Tulishushwa kwenye gari na kuanza kuingizwa mle ndani. Machozi yalikua bado yananitiririka bila kikomo. Wakati tunaingia mle ndani tayari wafungwa wengine walituona. Wakaanza kuimba kwa makelele.
"WAKE ZETU WAMEKUJA"
"WAKE ZETU HAOO WAMEKUJA"
Nilishituka kiasi ila tukazidi kusonga mara kuna kikundi kikaniona ya kua nalia basi walinifuata na kuanza kuniimbia.
"MAMA HUYOOO KATOKA SHAMBANI.
NA MKUNGU WA NDIZI HUYO
MAMAA MAMAA MAMAA"
Nilijisikia vibaya sana kwakweli lakini ningefanya nini unadhani. Maisha yalikua yamebadilika na kua machungu kwangu. Sikua na ndugu mwenye uwezo japo wa kunitafutia mawakili wa kunitetea. Nilikua kama yatima. Askari akanifungua pingu na kuniachia huku akisema utamwona nyapara upewe nguo zako za huku. Nikamwuliza nyapara ndo yupi. Badala ya kujibiwa nilipigwa bonge moja la kofi. Kisha akanitemea mate na kuendelea kuwafungua pingu wale wengine. Nilihisi kudharirishwa sana mbele ya wafungwa wale kilikua kitendo cha dharau kwani kuuliza ilikua haki yangu. Afisazi mzima natemewa mate napigwa kofi? Kweli thamani yangu ilikufa.
Baada ya askari kuondoka nikawa nasogea mbele huku wafungwa wakinizomea na kunibeza. Kwa bahati nikamwona kijana mmoja niliwahi kumkamata siku za nyuma. Nikamfuata nikamwuliza nyapara hapa ndo yupi? Aliniangalia akanipandisha na kunishusha kisha akasema we msenge nini? Nitolee jamu hapa mwehu wewe. Kisha akanionyesha sehemu ya kuelekea kwa kuninyoshea kidole. Kwa mbali nikamwona kama mtu namfahamu hivi.
Nilianza kusogea kwa kasi na kumfuata. Mungu wangu huyu alikua ni jambazi sugu miaka hiyo ya nyuma na nlimkamata mwenyewe. Sasa leo namkuta ni nyapara haaa!! Nilipigwa na butwaa sana. Nikasogea mpaka nafika ile kuniona tuu alikunja sura kisha akaanza kutoka kule alikokuwa na anakuja kwangu niliko. Alikua sasa kanenepa kiasi na kujazia misuli tofauti na alivyokuwa mwanzo. Nilisimama ili nione atafanya nini.
Kwa bahati mbaya alifika akanipiga ngumi shavuni na kunifanya nimwage damu. Hakufanikiwa kunichokoza kwani niliamua kumkalia kimya. Akanipiga tena pia sikujibu nilibaki kimya hali ile ilimfanya hata yeye kuogopa. Akatoka na kugeuka nyuma kisha akarudi na kunitupia zile nguo za jela. Nilivaa nguo zile kisha nikaingia sehemu moja hivi na kuamua kukaa. Nilikua nimechoka sana na zaidi nilikuwa nawaza maisha ya watu huko nje.
Nikiwa pale usiku uliingia siku ile sikukala nilibaki nimekaa. Wenzangu walilala lakini mimi siku ile sikuweza. Usiku nilishuhudia mambo mengi sana kwa wale wafungwa ikiwemo baadhi yao kuvuta sigara, wengine mpaka bangi. Najua vile vitu haviruhusiwi gerezani hivyo ilikuwa ni makosa. Pia nilishangaa vile vitu vinaingiaje jela. Lakini zaidi nilishuhuhdia baadhi ya wanaume wakigeuzana wenyewe kwa wenyewe na kufanya mapenzi. Kilichoniuma ni kuwa kuna wengine walionekana kulazimishwa na wababe wa mle ndani. Sikutaka kufanya chochote nilikua bado nina yangu kichwani nayawaza na kuyafikiria.
Usiku ule ukapita na kukakucha hapo ndipo tuliamshwa. Tuliitwa ku pewa uji. Tulikunywa na uji ule haukua na sukari hata kidogo. Sikujali hilo mda wote nilikia mpole na mtulivu na nisiyeongea nabyeyote. Niliwaona wafungwa lukuki waliokua wamekamatwa kwa mikono yangu. Wengine walinitambua na wakapania kunifanyia kitu kibaya. Wengine hawakunitambua. Niliendelea na ukimya bila kusemezana na yoyote.
Nakumbuka tulienda sehemu moja hivi kulikua na kazi ya kupasua mawe. Tulikua tunaandaa kokoto. Kuna askari magereza mmoja akapita karibu yangu na kunipiga mjeredi. Niligeuka nikamwuliza kosa langu nini? Akacheka, hapo ndipo nikaona huyu hanijui nikatupa nyundo chini nikamfuata kisha nikamkunja mara askari wengine wakaja kunitoa. Nilikua nina sifa moja mikono yangu ilikua na nguvu sana. Nikimkaba mtu hawezi kutoka. Basi nilimkaba yule mtu shingoni Maaskari walipiga lakini wapi? Walinigonga na virungu lakini sikuachia. Basi mmoja akanigonga na nyundo kichwani huku nyuma na kisha nikaanguka. Na kumwachia yule askari.
Nilichukuliwa nikarudishwa jela nikalale. Nililala mpaka usiku. Ambapo wafungwa wote walikuwa wamerudi tangu jioni. Kuna kikundi niliwasikia wakijadili kunigeuza mke wao usiku ule. Walikua wakipangiana zamu huku wakijua mimi nimelala usingizi. Wakasema kwanza huyu bikra tangu afike hajaguswa na mtu. Ni jana ndo kafika hivyo nitaanza mimi wengine mtafuata. Mmoja akadakia masta usiwe na shaka. Basi wakaongea na kukubaliana mi nikiwa kimya. Usiku ule ulizidi kusonga mara kukiwa kumetulia sana nadhani ilikua ni usiku mnene. Tayari baadhi ya wanaume walianza kutembea tembea mle ndani. Mara mimi nikashtuka nashikwa mikono na miguu kisha____________ ______________________________
______________________________ ______________________________ ______________________________ ______________________________ _Usikose sehemu ya 31

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:
Post a Comment