» » Serikali yafuta ushuru wa gesti Yatangaza Neema Kwa Wafanyabiashara

Serikali imetangaza kufuta ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala wageni.

Hayo yameelezwa jana (Alhamisi) bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango wakati akiwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18.

Pamoja na ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali zinapopatikana huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.

Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.

Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles