» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 37 NA 38.


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 37.
Tulipoishia, Moyo ulilipuka paah! Pale nilipomwona Uso kwa uso Zabroni Makweka. Hasira ikanivamia. Taratibu nikajikuta nagadhabika ile nataka kuinuka mara nimasikia mlio wa mtu akiiandaa bunduki kufyatua risasi. Mara ghafla____Enda nayo............Nikawekewa mitutu ya bunduki isiyo pungu minne. Kumbe kulikuwa na kundi la watu nyuma yangu. Nilishindwa hata kujitingisha wala kufanya lolote kwani nilikuwa katikati ya majambazi. Nilimwangalia Zabroni kwamakini nikamwona anatabasamu. Kisha nikasikia sauti nyuma yangu ikisema uko chini ya ulinzi. Tumekuta maiti nje ya nyumba yako! Pili umetoroka jela. Hivyo unatuhumiwa uko chini ya ulinzi inua mikono juu. Sikua na ujanja zaidi ya kuinua mikono tuu.
Nikafungwa pingu kisha nikamwona Zabroni akiagana na wale maafande na kuondoka. Nilimeza mate ya hasira funda moja kisha nikamwona akipotea na suti yake. Ila kuna kitu kilikuwa kinanichanganya sana. Ni mwonekano wa Zabroni yaani alikuwa kama mimi kwa kila kitu. Sura mpaka sauti. Nilijiuliza maswali mengi sana. Nikweli duniani wawili wawili lakini ile ilizidi. Hata sauti hata kutembea na kama ingekuwa sura ya bandia ingekuwa hata kuna mwelekeo wa kupishana baadhi ya vitu. Sasa kwa pale hapana lazima kuna namna? Huyu Zabroni makweka ni nani? Mbona sielewi?
Nilikuwa najiuliza hayo maswali wakati maafande wakiniondoa pale. Tulitoka tukatembea umbali kiasi nikashangaa badala ya kunipeleka kituoni wameanza kunipiga. Hapo ndipo waliharibu. Niliingiwa na hasira nikaanza kupigana huku nina pingu mkononi. Nilikuwa narusha mikono yote kwapamoja mpaka nikawa naelekea kuwashinda. Hapo ndipo wakatoa bunduki na kuanza kunipiga kwa vitako vya bunduki bila kikomo. Nilichezea kichapo cha maana mpaka nilikuwa sijielewi.
Nilivuja damu nyingi sana kisha wakanichukua na kunipeleka kwenye jalala fulani wakanitupa hapo wao wakatoweka. Nilikuwa siwezi kusimama wala kufanya lolote. Nilibaki naugulia maumivu pale jalalani huku mikononi nikiwa na pingu. Nililia sana nikakufuru nikaona bora kufa nikapumzike. Mateso gani haya yasiyokoma. Mbona nchi yangu imejaa watu wasaliti? Naipigania naipenda naililia lakini hakuna anayependa mapambano yangu. Tazama naumia kisa nchi lakini naishia kulala kwenye jalala tena nikiwa na pingu nini maana yale. Je ni kweli Serikali imeshindwa kuniokoa. Kwanini?
Hapo ndipo nikakumbuka wimbo tuliokuwa tunaimba wakati tuko depo. Hata shuleni tuliuimba sana.
"Tanzania Tanzania nchi
Yenye mali nyingi watu
Wengi wa ulaya
Wanaililia sana"
Nilipomaliza kumbukumbu ya wimbo huu nilikuwa nikitafakari. Kama Tanzania ina mali nyingi mbona wanafaidi wachache? Nilijikuta nimepoteza fahamu na sikujua kilichoendelea mpaka hapo niliposhtuka nikiwa nimezungukwa na njemba za uhakika. Nilipoinuka mmoja akanisukuma nilale. Kisha mmoja akaja na kunichoma sindano nadhani ilikuwa ya usingizi kwani nililala tena. Niliposhtuka mara ya pili nilikuwa niko mwenyewe sikumwona mtu.
Nilijiona nipo kwenye chumba fulani kina urembo urembo. Nilitaka kuinuka nitembee lakini maumivu ya kipigo yalinizidia mara nikasikia sauti ya kike ikiniambia pole kaka pole. Akatokea mrembo mmoja mwenye asili ya kihindi alikuwa mzuri haswaa. Akanambia jamani hebu pumzika kwanza una harakia wapi kakangu? Nikamwangalia kwa jicho kali kisha nikamsukuma halafu nikamwambia. Nitoe humu nitoe niko wapi? "Take it easy" sauti nyororo iliongea huku akinisogelea. Kisha akasema hivi kama ningekua mbaya kwako ningekuacha hai mpaka mda huu?
Kwanini unanihukumu kaka bila kunisikiliza? "Any way" nimekusamehe bure lakini! Enheee unajisikiaje? Nilijikuta naanza kulegeza misimamo yangu kwani nikahisi huenda ni nesi na ameamua kun isaidia halafu mimi namsukuma. Nikajikuta nimelegea nikamjibu, najisikia maumivu mwili wote! Akasema polee. Nikajibu ahsante kisha nikamwuliza hapa niko wapi na wewe ni nani? Akajibu usijali utajua ila kifupi sisi ni wasamalia wema na tulikuona umezimia pale jalalani tukaamua kukusaidia. Kwahiyo hapa ni wapi? Akajibu usiwe na shaka kuwa na amani kakaangu sawa eee? Nikaamua kujibu sawa ila nilikuwa sijaridhika.
Siku zilisonga nikihudumiwa mule ndani na yule dada bila kumwona mtu yeyote mwingine. Hali ile ilianza kunipa wasiwasi lakini chaajabu ni kuwa yule dada alikuwa akinihudumia kwa kila kitu ila tuu alinikataza kutoka lakini kuna siku alinitoa nikashangaa kiasi vya nje. Yalikuwa maeneo mapya kabisa kwangu. Alinifanyisha mazoezi mengi mpaka nikawa mzima kabisa. Basi kuna siku akaja na passport ya kusafiria na akanambia kuna mizigo natakiwa nimsaidie kumpelekea Afrika ya Kusini.
Kwakuwa alinisaidia sana sikuona sababu ya kukataa. Nilimkubalia na mipango ya safari ikafanyika kisha nikatakiwa kuwahi uwanja wa ndege. Nilifika kiwanja cha Mwl Julius na kukaguliwa kisha safari ikaanza. Chaajabu ni kuwa mizigo niliyotakiwa kusafirisha ilikuwa imetangulia kwenye ndege bila kukaguliwa hili lilinipa mashaka. Baada ya Kufika Afrika ya kusini kuna watu walikuja kunipokea lakini kuna mmoja kati yao alinishtua kiasi. Kwani alikuwa kana namfahamu hivi na kama ni miongoni mwa majambazi niliowahi kuwakamata. Nilivumilia nikazhindwa nikaamua kumfuata na kumwuliza___________________________________ _________________________________________________________________________________________________________
______Cheki na mm sehemu ya 38 nikupe yaliyojiri hapo. Naona mambo bado magumu daaaah ni sheeda.

SEHEMU YA 38.
Tulipoishia, Kwani alikuwa kama namfahamu hivi na kama ni miongoni mwa majambazi niliowahi kuwakamata. Nilivumilia nikazhindwa nikaamua kumfuata na kumwuliza_______Songa nayo........Hey habari yako mkuu? Aligeuka na kunijibu "can you speak English please? Oooh sory i didn't know that you do not undeestand swahili. What is your name by the way? Akajibu Am John born here in South Africa. Nikamjibu okey i just wanted to know that! Nice to meet you mr John! Akajibu you are welcome. Nikaamua kuachana naye na kurudi nyuma kidogo. Ndani ya kundi lote waliokuja kunipokea nilikuwa simfahamu hata mtu mmoja. Ila kulikuwa na Watanzania watatu hao ndio nilikuwa naongea nao kiswahili. Basi tulitembea mpaka tukafika eneo fulani hivi palikuwa na jengo la kifahari hapo ndipotulitakiwa kuingia na mizigo yetu.
Tuliingia ndani huku nikiwa na wasiwasi wa kugeukwa lakini chaajabu palitawala amani sana. Kisha baada ya siku mbili walinikabidhi pesa nyingi sana zilikuwa ni dola za kimarekani. Niliambiwa nizifikishe kwa yule dada. Nilishtuka sana kwanini dada yule aliniamini kiasi kile? Je hakuwaza kama naweza kimbia nazo? Au nategwa kupimwa uaminifu wangu? Nilipokuwa najiuliza jinsi ya kupata tiketi kurudi bongo nikaambiwa tiketi tayari. Mmmh niliguna kisha nikawauliza kama naweza kuiona.
Walikuwa hawana tatizo wakanipa. Nkaiona. Siku ya pili walinipeleka uwanja wa ndege na kuhakikisha nimepanda kisha wao wakaondoka. Nilikuwa najiuliza hivi mbona nanyenyekewa sana? Hapana huenda kuna kitu nyuma ya Pazia. Nilifika Tanzania na nikaamua kuonyesha uaminifu wangu nikampelekea yule dada zile pesa kisha akanishukuru sana na akanipa kiasi kingi tuu. Nilishangaa sana. Maisha yakaanza kubadilika sana kwa upande wangu. Nilifanya safari za Afrika ya kusini mara kadhaa bila kujua napeleka nini? Kwani mizigo nilikuwa nafika iko uwanja wa ndege tayari na pia nikifika afrika ya kusini nawakuta jamaa wanaichukua mojakwamoja toka kwa wahudumu. Kuna siku nikaamua kumuuliza yule dada ni nini huwa napeleka Afrika ya kusini.
Ndipo akanisogelea na kuniuliza hivi Yuu katika hii dunia umefanya mema mangapi? Nikamjibu mengi tuu! Akaniuliza na umefanya mabaya mangapi? Nikamjibu mengi pia? Akaniuliza je mazuri na mabaya ukilonganisha yepi Mengi? Nikamjibu mazuri? Akasema na katika hayo mazuri uliyofanya umelipwa nazuri mangapi? Nikamjibu machache! Basi akasema ikiwa umelipwa mazuri machache na umefanya mengi je ikitokea kuna baya litakalokulipa mazuri utaliacha?
Yalikuwa maswali yenye hoja za msingi ndani yake. Nikamjibu kumbe kuna ubaya unaolipa mazuri? Akajibu "absolutely" kwani si kila mema unayofanya utalipwa mema kwani wewe nimekukuta umezimia pale ulikuwa umelipwa ubaya je ulifanya ubaya? Nikamjibu hapana ninapigania nchi yangu? Waah je nchi inatambua jitihada zako, I mean viongozi wanashirikiana na wewe? Nikajibu hapana kwani vipi? Akajibu Yuu hakuna kitu kizuri kama uzalendo lakini siyo kwa nchi kama hii yakwetu. Viongozi wake wamejaa ubinafsi, Ni wasaliti, wanafiki, Wanasiasa waongo! Yuu tafakari haya. Tuna milima miwili mirefu sana Africa yote Meru na Kilimanjaro watalii wanajaa kila leo pesa zimeenda wapi?
Tuna mabonde ya kuweza kulima mpunga na kuzalisha vizuri ni makubwa sana, bonde la usangu, bonde la kilombelo, na mengine lakini bado tunategemea mchele Japan, Tuna gesi, mafuta, madini, maliasili chungu nzima. Wanyama wa ajabu. Kwanini tunaumia? Baadhi ya viongozi siyo wazalendo walimfunga baba yangu wakamfunga mama. Niliteseka sana. Hawakuwa na hatia kisa kutetea taifa. Alipoongea hivo ndipo na mimi nikaanza kuwaza kuwa nateseka kupambana lakini hakuna kiongozi ajuaye mchango wangu. Nimefungwa nimeuliwa ndugu na jamaa. Nimepigwa na polisi wa nchi yangu kwanini? Ni nini nimepata?
Nikamgeukia yule dada nikamuuliza unamanisha nini dadangu? Namanisha tafuta pesa Yuu hata hao wanaokusumbua unashindwa kuwalipa kisasi kwasababu ya umasikini. Aliongea vitu vingi ambavyo vilinihamisha kimawazo na kujikuta nakuwa mpole na kusikiliza ni nini anaongea. Baada ya mda akamaliza na kuniambia yeye pia anafanya vile ili kupata pesa kisha alipe kisasi mahali. Je uko tayari kuungana na mimi Yuu? Nikajikuta namjibu ndiyo! Yule dada alikuwa ametumia akili sana kuniteka kimawazo hata hakutumia nguvu. Hivi ndivyo ujuzi na weledi wa mtu hutumika.
Basi tayari nikaingia kwenye biashara zisizo halali za kuteketeza watanzania wenzangu. Nikaanza kuingiza na kutoa madawa ya kulevya. Sitasahau siku moja tukiwa Afrika ya kusini. Kulikuwa na uwekwaji wa mihuli ya chama hilo kubwa la biashara haramu. Ilikuwa tunawekwanalama sehemu ya paja na chuma cha moto chenye maandishi. Mpaka kufikia pale maana yake ni kuwa wewe umepandishwa daraja unaweza fanya biashara nyingi sana haramu. Muhuri huo ninao mpaka sasa na hautakaa ufutike kwani lilikuwa ni shimo kwenye paja langu. Hali ile ilinifanya kuka kiapo na kulitumikia vyema kundi lile la ujambazi.
Kuna kitu kilikua kinanitatiza ni kuwa ule muhuri ni kama niliwahi kuuona kwa Peris ambapo alinidanganya kuwa aliunguzwa na kifaa cha moto kwa bahati mbaya. Nilikumbuka pia kuwa kuna mhalifu mmoja nilimwona na alama ile. Kwakuwa nilishakata shauri nikaamua kuachana na hayo. Kisha nikaendelea na kazi yangu nikishirikiana kwa ukaribu sana na yule dada. Tulitengeneza pesa nyingi sana kwani tulikuwa mpaka tunasafirisha watu kuwapeleka nje ya nchi kuwauza wengine walikuwa wakifanyishwa umalaya. Mi sikua najali hayo mimi nilikuwa najali kama napata pesa tuu basi. Kuna siku nikiwa uwanja wa ndege wa mwl Nyerere Kuna askari wawili walikuwa wakiniangalia sana. Nikiwa nataka kuwakwepa nikaona wanasogea karibu yangu. Wakafika kisha_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Tukutane sehemu ya 39 nikupe yaliyojiri! Nawapenda wote. Nawatakia siku njema na Mungu awabariki. Chaooooo

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles