SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 34.
Tulipoishia, Nikamjibu sawa kisha nikausukuma ule mfuniko taratibu na kumwangalia yule jamaa. Woga ulikuwa umenitawala sana. Nikachomoa kichwa kidogo kisha nikachungulia nje nione kama kuna usalama mara nikasikia______Songa sasa.......... Vipi kaka kuna usalama? Alikua ni yule mjinga akiuliza? Nikamjibu sijamwona mtu hapa mpaka sasa akajibu sasa toweka uende. Nikamjibu sawa sasa we vipi akajibu mi nabaki hukuhuku uraiani mateso. Ikiwa utahitaji msaada wangu utanifuata basi sawa eee? Tukaagana pale ila mimi roho yangu ilikua bado ina kinyongo naye nilitamani sana kumwua. Lakini nikasema nitamrudia siku zijazo.
Nikainuka na kufunika mfuniko kisha kugeuka nianze kukimbia. Mara nikashtukia nimewekewa mtutu wa bunduki kichwani na askari. Vipi kijana waenda wapi? Nikatulia kiasi huku nikimwangalia kwa wizi nikamwona kazubaa. Nikainua mikono haraka na kuvuta bunduki kisha nikamwelekezea na kummiminia risasi mpaka zilipoisha kwenye bunduki. Nilikuwa na hasira sana na kila mtu aliyeonekana kunizuia mipango yangu. Nilipomaliza nikatupa bunduki pale kisha nikaondoka kwa mbio za kunyata na kutokomea. Nilifika sehemu nikajificha na kusubiri mda uende. Nilikaa hapo mpaka usiku. Usiku nikaanza safari mpaka nyumbani ambako nilipofika nilikuta nyumba katika usalama kwani Oscar alikuwa akiilinda. Alishtuka sana kuniona kabla ya miaka mitano kuisha. Nikaingia ndani na kutoa zile nguo za jela kisha nikapumzika mpaka asubuhi.
Nilipoamka nilivalia nguo zenye kuficha vizuri sura yangu. Nilivaa miwani ya rangi nyeusi na kofia kisha nikavalia koti fulani. Ilikua ngumu kwa mtu kunitambua kirahisi. Nikachukua risasi za kutosha na bastola na kujihami kiasi. Nilikua najua pakuanzia. Nilianza safari na oscar na kufika sehemu moja huko mwananyamala. Ndiko nilielekezwa kuwa kuna ngome nyingine kule. Nilipofika niliona shuhuli zikiendelea katika ile nyumba. Yaani ilikua ni nyumba ambayo nje ina wapangaji lakini ndani kuna shughuli za kihalifu. Nilipoingia sikuuliza nilianza kumwaga risasi bila huruma. Oscar alishiriki vizuri sana mpaka tukaingia ndani. Tulikuwa tumeshauwa watu wengi sana.
Baada ya kumaliza hilo tulitoweka eneo la tukio na kurudi nyumbani. Kwakuwa nilikuwa sina kitu mfukoni yaani pesa ilinibidi nianze ubabe ili kufanikisha azma yangu ya kulipa kisasi. Usiku ule nilisikia taarifa ya habari wakisema kuna majambazi wamevamia nyumba moja na kuua watu wasio na hatia. Nilizidi kujisikia vibaya kwani niliona uovu unazidi kutetewa. Hivi majambazi ambao polisi imeshindwa kuwatia nguvuni halafu wanaitwa watu wasio na hatia.
Nikamwambia Oscar zima tv! Akauliza kwani vipi bro? Nikamjibu zima zimaa! Haiwezekani majambazi wazurure na kula raha kisha tusio na hatia ndo tunaonekana waovu na kuswekwa jela kutumikia vifungo visivyotuhusu. Nawachukia sana hawa wajinga. Basi Oscar akazima tv kisha mi nikanyanyuka na kuingia chimbani na kuamua kulala. Mda ukasonga sana usiku ukapita asubuhi kulipokucha nikawa nawaza jinsi ya kupata pesa ya kutumia. Nilisugua kichwa na kupata jibu. Nikainuka na kwenda kwenye benki moja hivi hapa jijini Dar es salaam. Nikaingia na kuomba kuonana na meneja. Niliruhusiwa nikaomba kuonana tukiwa wawili tuu. Pia nikakubaliwa.
Lilikuwa kosa kubwa wamelifanya. Huku nyuma ndani ya ofisi ya meneja nilimbadilikia na kumuhitaji kuokoa uhai wake kwa milioni mia mbili. Hakuwa na jinsi alinionyesha boksi moja lilikuwa limejaa pesa. Baada ya kulikagua chini ya uangalizi wa meneja huku nimemshikia bastola. Nikaona ni pesa nyingi sana. Bastola yangu nilifunga kifaa cha kuzuia sauti hivyo nikamzima meneja wa benki kimyakimya. Sikuwa na jinsi roho iliniuma kuua watu wasio na hatia lakini ningefanyaje unadhani. Hakuna aliyezaliwa muhalifu ila mazingira na m ifumo inaweza kukufanya kuwa muuaji na muhalifu mkubwa. Nikachukua mfuko wa kaki pembeni nikajaza pesa kisha nikajiridhisha na kuamua kuondoka.
Nilijihakikishia ya kuwa niko vizuri nikatoka. Mpaka natokomea eneo lile hakuna alinishitukia. Nilifika nyumbani na kuamua kuacha pesa bila kuhesabu. Jioni ilipofika nilihesabu na kukuta ni milioni 250. Nikafurahi na kuona kumbe zoezi langu nitakamilisha vizuri bila wasiwasi. Nikapanga safari niende kwanza kijijini nikawaangalie wazazi hali zao na kisha nirudi. Nilitafuta gari la kununua haraka siku ya pili nikawahi kijijini kwetu. Niliwakuta wazazi wangu katika hali mbaya sana. Niliumia sana walinikumbatia tukalia wote machozi. Ilikuwa kama msiba lakini kumbe siyo. Haki ilidhulumiwa kwangu pekee lakini iliwaathiri wengi sana. Tuliumia sana mimi na wazazi wangu. Baada ya majonzi na maombolezo ya mda mrefu tukakaa na kujadili mambo mengi sana ya maisha. Niliwasimulia walinipa pole. Nikawaambia azma yangu. Wakafurahi sana.
Baada ya kuongea sana kuna vitu nilihitaji kuchukua ndani ya gari. Na wakati nafika kwenye gari nilishtuka milango yote ya gari iko wazi. Nilishangaa kwani nilikuwa nimeifunga. Nikasogea na kufika nikaangalia ndani nikaona kuna bunduki tatu aina ya AK 47, pembeni kulikuwa na risasi nyingi sana. Kisha kulikuwa na barua. Wakati natafakari Kuichukua barua ile mara nikasikia mlio wa risasi ukiwa umetokea walipo baba na mama. Nilishtuka nikageuka na kukimbilia mara nikaona______________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Tukutane sehemu ya 35 tujue yaliyojiri huko kijijini! Nawapenda wote nawatakia kazi njema.
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 34.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment