» » Shambulio darajani London

Watu wakikimbia katika barabara ya Borough High Street kusini mwa Daraja la London

Haki miliki ya pichaPA
Image captionWatu wakikimbia katika barabara ya Borough kusini mwa Daraja la London
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadha kujeruhiwa katika tukio lililohusisha watu kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu katika eneo la Daraja la London.
Polisi wa Uchukuzi Uingereza wanasema walipokea taarifa za watu kugongwa kwa gari katika daraja hilo.
Maafisa wenye silaha walitumwa eneo hilo baada ya watu walioshuhudia kusema gari la rangi jeupe lilivurumishwa kutoka kwenye barabara na kuwagonga watu waliokuwa wakipita.
Maafisa walitumwa pia katika Soko la Borough, ambapo inadaiwa watu walishambuliwa na kudungwa visu.
Polisi Jijini London, wanasema kuwa visa hivyo viwili ambavyo vimesababisha kifo cha mtu mmoja na zaidi ya watu 20 kujeruhiwa, vinachukuliwa kama vitendo vya kigaidi.
Ghasia zilianza baada ya gari moja kuingia ndani ya umati wa watembeaji miguu katika daraja kuu jijini London.
Aliyeshuhudia ameiambia BBC kuwa, aliwaona watu watatu wakiwa na visu, wakikimbia kutoka katika daraja hilo, kuelekea eneo moja kuliko na soko la Borough.
Anasema kuwa watu hao watatu walianza kuwadunga visu watu kiholela barabarani.
Muda mfupi baadaye, polisi waliokuwa na silaha wakajibu shambulio hilo, huku milio ya risasi ikisikika.
Watu 20 wanasemekana kupelekwa katika hospitali sita tofauti Jijini London.
Maafisa wa polisi wenye silaha wametumwa barabara ya Borough High StreetHaki miliki ya pichaPA
Image captionMaafisa wa polisi wenye silaha wametumwa barabara ya Borough High
Polisi na magari ya kubebea wagonjwa katika upande wa kusini wa Daraja la London
Image captionPolisi na magari ya kubebea wagonjwa katika upande wa kusini wa Daraja la London
London bridge
Image captionRangi za taa za magari ya maafisa wa huduma za dharura zikioneakna eneo la Daraja la London
Daraja la London kwa sasa limefungwa.
Mabasi yanaelekezwa kwingine. Daraja la Southwark lililoko karibu pia limefungwa.
Shirika la Uchukuzi London (TfL) limesema babarara ya Borough High pia imefungwa, na taarifa zinasema maafisa wa polisi wenye silaha wameonekana maeneo hayo.
Mwandishi wa BBC Holly Jones aliyekuwepo katika daraja hilo wakati wa kutoka kwa tukio hilo, anasema gari lililohusika lilikuwa linaendeshwa na mwanamume na lilikuwa linaenda kwa kasi ya karibu maili 50 kwa saa.
"Alilipinda gari karibu nami na akagonga watu watano au sita hivi. Aliwagonga wawili mbele yangu na kisha wengine watatu waliokuwa nyuma yangu," Bi Jones ameambia BBC.
Watu hao watano au sita wanatibiwa, amesema.
Bi Jones anasema gari hilo lilikuwa linasafiri kutoka katikati mwa London na lilielekea upande wa kusini wa mto.
Anasema baadaye aliona mwanamume akikamatwa na kutiwa pindi na maafisa wa polisi.
Bi Jones anasema mwanamke Mfaransa ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Tukio hilo ambalo linatukia majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa pale mhanga mmoja wa kujitolea kufa, alipojilipua ndani ya uwanja mmoja wa burudani huko mjini Manchester, limelaaniwa na viongozi mbalimbali duniani.
Tweet from LASHaki miliki ya pichaTWITTER
Maafisa wa Magari ya kuwabeba wagonjwa wa London, moja ya idara za kwanza kuzungumzia tukio hilo, walisema wanashughulikia kisakikubwa eneo la Daraja la London na kuwatahadharisha watu wasielekee eneo hilo.
Aerial map of scene


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...