» » Anna Mghwira ateuliwa kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro

Mghwira ndiye mwanamke pekee aliwania urais Tanzania

Image captionMghwira ndiye mwanamke pekee aliwania urais Tanzania mwaka 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Bibi Anna Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Saidi Meck Sadiki aliyekuwa mkuu wa mkoa huo.
Bi Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015.
Amekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, chama kichanga zaidi Tanzania kilichoundwa 2014.
Mghwira, 56, anatoka mkoa wa Singida. Babake alikuwa diwani na kiongozi chama cha Tanu na baadaye CCM.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa mkuu wa oparesheni na mafunzo wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania.
Halikadhalika Rais magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omar Juma Kaniki kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omar Juma alikuwa mkuu wa jeshi la polisi.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles