» » Marekani yachunguza shambulio kubwa la mtandao

Siku za hivi karibuni uvamizi wa mitandao umeshika kasi duniani

Image captionSiku za hivi karibuni uvamizi wa mitandao umeshika kasi duniani
Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.
Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.
Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.
Serikali ya Ukraine iliweka aina hii ya uvamizi wa mtandao uliofanywa hivi karibuni
Image captionSerikali ya Ukraine iliweka aina hii ya uvamizi wa mtandao uliofanywa hivi karibuni
Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika.
Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.
Huku ikisema hakuna uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika.
Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles