» » CCM Walaani Matamshi ya Lowassa......Waitaka Serikali Imchukulie Hatua


Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kauli za kichochezi na zakidini zilizofanywa na mmoja kati ya mwanasiasa nchini, zenye lengo la kuwafitinisha watanzania.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM ndugu Humphrey Polepole amebainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, huku akiiomba serikali ikithibitika mtu amekosea serikali isiwe na ajizi kuchukua hatua kwa aina ya mtu huyo.

Siku ya Jumanne na leo Alhamisi,  aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amehojiwa na Jeshi la Polisi kwa kilichodaiwa kuwa ni maneno ya kichochezi aliyoyatoa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati alipohudhuria Futari iliyokuwa imeandaliwa na Mbunge Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Katika hatua nyingine, Polepole amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaunga Mkono Kauli ya Rais Magufuli ya kutorudi masomoni kwa wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shule kwenye mfumo rasmi wa Elimu.

Polepole amesema kuwa wanafunzi waliopata ujauzito hawataweza kurudi shuleni kwenye mfumo rasmi isipokuwa kwenye Mfumo wa elimu ya watu wazima.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles