» » Waziri mwenye umri mdogo zaidi Somalia auawa

Abas Abdullahi alikuwa katika gari hili na aliuawa akitokea katika shughuli zake

Image captionAbas Abdullahi alikuwa katika gari hili na aliuawa akitokea katika shughuli zake
Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia.
Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.
Abas Abdullahi hakuwa na uzoefu katika siasa lakini alipendwa na wengi
Image captionAbas Abdullahi hakuwa na uzoefu katika siasa lakini alipendwa na wengi
Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri.
Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.
Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles