» » " Wasukuma Tutaziloga Ng'ombe Zetu Ili Mtakaokula Mvimbe Matumbo" - Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku


Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi kumsifia hata kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii kwani yeye na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa Kanda ya Ziwa.

Musukuma anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza ng'ombe za watu jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la kujinufaisha wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa wataziroga ng'ombe zote ili wanaokula ngo'mbe hizo Dar es Salaam wavimbe matumbo.

"Napata shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya ziwa labda tulikuja kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya Ziwa hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa siku tatu tukamatiwe ng'ombe kwa kisingizio kwamba ni ng'ombe za Wanyarwanda wakati huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda wanawaambia toeni ng'ombe, mnaenda kukamata ng'ombe za Wasukuma halafu unazipiga mnada na mnada wenyewe unavyopigwa ni wa dili" alisisitiza Musukuma

Mbunge huyo aliendelea kuelezea namna watu wa Wizara ya Maliasili wanavyofanya minada hiyo huku wakiwaumiza wafugaji

"Yaani ng'ombe 600 unaambiwa ulete milioni tatu halafu wanatoa watu wao wa Ubungo sasa hapo nikupongeze kwa sababu gani? Tunajua mipango inayoendelea kwenye wizara yako na niliwapigia kabisa watumishi wako, wananiambia mliipenda wenyewe kwa kauli yake kama Mwenyekiti wa Chama kesho yake akapiga ng'ombe za watu mnada yaani ng'ombe 500 zinauzwa milioni tatu" alisema Musukuma

Joseph Msukuma aliendelea na msimamo wake

"Nataka nikwambie sisi Wasukuma sasa tumeamua na ninazungumza uelewe tutaziroga hizo ng'ombe mtavimba matumbo mnaozila huko Dar es Salaam, haiwezekani kwanini wanunuzi watoke Dar es Salaam peke yake yaani leo siku ya mnada watu wametoka na malori Pugu wamejuaje kama wanakuja kushinda kwenye minada. Mnatukamatia ng'ombe hivi hii serikali imekosa sehemu ya kukusanya hela mpaka mkanyang'anye ng'ombe za wafugaji haiwezekani Mh. Maghembe"

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...