» » Wasichana 82 wa Chibok, waachiwa huru na Boko Haram


Picha ya baadhi ya wasichana wa Chibok waliotekwa nyara muda mfupi mwezi Mei 2014

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPicha ya baadhi ya wasichana wa Chibok waliotekwa nyara muda mfupi mwezi Mei 2014
Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa 2014, wameachiwa huru.
Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.
Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie Hegarty kutoka Lagos.
Ramani ya Nigeria inayoonyesha mji wa mpakani wa BankiHaki miliki ya pichaTHINKSTOCK
Image captionRamani ya Nigeria inayoonyesha mji wa mpakani wa Banki
Mwaandishi wetu anasema kuwa, familia nyingi huko Chibok wamefurahia taarifa hiyo ya hivi punde lakini wapiganaji hao wa Boko Haram, wangali wakiwazuilia zaidi ya wanafunzi 100.
Ni sehemu ya maelfu ya watu ambao wametekwa nyara na wanamgambo hao, walioanzisha vuguvugu hilo miaka minane iliyopita.
Wasichana 21 walioachiwa huru Oktoba 2016Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWasichana 21 walioachiwa huru Oktoba 2016
Utekaji nyara huo ambao ulifahamika baadaye kama "Chibok girls" ulisababisha kilio kikubwa kote duniani na kampeini za kutaka waachiwe huru ikatanda kote katika mitandao ya kijamii.
Kabla ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
Idadi ya washukiwa wa Boko Haram ambao wameachiwa huru na utawala wa Nigeria, bado haijajulikana.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...