Kifo ni adui mkubwa wa binadam. Amekua mgeni asiyebisha hodi na hutokea popote na wakati wowote. Hachagui tajiri wala masikini, msomi na asiyesoma, warefu na wafupi. Kutokana na maumivu makali yanayoletwa na kifo, Imani nyingi zimeibuka zikiwa na mafundisho mbalimbali juu ya Kifo. Nyingi zikiwa na lengo la kuwafariji wafiwa, zingine ni kukuza umizimu. Mafundisho makubwa yaliyotawala kwa sehemu kubwa ni juu ya kutokufa kwa ROHO. Kwamba mtu anapokufa Roho huenda mbinguni kwenye raha, au Kuzimu kupata adhabu ya milele. Imani nyingine ni ile ya kuzaliwa upya (Reincarnation) kwamba kama mtu atatenda mema akifa atazaliwa tena akiwa na maisha mazuri katika familia tajiri, au hata ya Kifalme. Lakini mtu akitenda mabaya atazaliwa akiwa mtu duni au hata kiumbe kingine kama mjusi, chura nk. Imani nyingine ni ile inayoamini kwamba kifo ni usingizi. Kwamba mtu anapokufa hupumzika kwa muda hadi Yesu atakaporudi na kuwafufua wapate Kuurithi uzima wa milele, na wengine hukumu ya jehanam.
Pamoja na Imani zote na zingine sijataja, ni bora kuangalia fundisho la Biblia juu ya hali ya wafu. Wakati Fulani tunaguswa na misiba mathalan umefiwa na Mke au Mume, mtoto au rafiki wa karibu, ukiwa katika wakati mgumu Unatarajia walau sauti inayokuhakikishia kwamba Marehem yuko sehem salama, anapata raha. Lakini je tungependa kusikia faraja ya uongo au ya kweli ambayo ni sawa na maandiko Matakatifu?
Nilihudhuria ibada moja ya mazishi ambayo ilianza kwa muziki wa taratibu. Baada ya kusoma Maandiko na kuomba Mchungaji alianza kuhubiri. Aliwahakikishia waombolezaji kuwa marehemu alikuwa hajafa kabisa alikuwa mzima na alikuwa mbele za Mungu. alikuwa akitazama kutoka mbinguni kila kilichokuwa kinaendelea katika ibada hiyo ya mazishi. Marehem alizaniwa kuwa yuko kwenye hali bora Zaidi ya maisha.
Kwa kuanza Ufafanuzi wa Biblia kwanza tufaham nini maana ya kifo. Kamusi ya Oxford inaandika “End of something” mwisho wa kitu. Ili kupata ufafanuzi mzuri kwanza tujue nini kinamfanya mtu kuwa HAI. Uhai ni Mwili jumlisha pumzi “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai”. Mwanzo 2:7. Tazama hii UHAI=Mavumbi+Pumzi. KIFO=Mavumbi-Pumzi ya Uhai.
Imani nyingi hata Wakristo zinafundisha kuwa Kuna Mwili, Kuna pumzi, na nafsi (Roho isiyokufa). Biblia inaandika “akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai” Hivyo mtu anapokufa anarudi kuwa mavumbi. Mwanzo 3:19 “kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” Huko mavumbini miili itapumzika hata Yesu atakaporudi mawinguni. Jifunze mafungu yafuatayo ili kuelewa Hali ya wafu. hatimaye uwe na tumaini la kweli katika Kristo. Usikubali kudanganyika wakati ukweli huu umewekwa wazi kabisa, hakuna toharani wala pagatory badala yake mafundisho kama hayo yanatumiwa na ibilisi ili kupalilia umizimu. Kwamba unaweza kuwasiliana na ndugu aliekufa, au akawatokea wakati Fulani. Hizo ni Roho zidanganyazo Biblia inasema. Soma 1samweli 28:7-14
Yohana 11:11-14 “Yesu alifananisha kifo na usingizi” Biblia inafananisha kifo na usingizi Zaidi ya mara 50.
1Thesalonike 4:15, 16 “wale waliolala katika Kristo watafufuliwa atakapokuja”.
Yohana 5:28, 29 “Kuna ufufuo wa aina mbili”. Wa uzima na mauti.
Mwanzo2:7 “Mungu alimuumba mtu kwa mavumbi ya ardhi na kumpulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa nafsi hai. Mungu hakuweka nafsi ndani ya mtu kama walimu na wahubiri wengi wanavyotufundisha. Muhubiri 12:7 “Mwili huyarudia mavumbi na Roho humrudia Mungu. Biblia haisemi nafsi humrudia Mungu, bali Roho.
Ayubu 27:3 “Roho ni sawa na pumzi au uweza wa Mungu uletao uhai”.
Zaburi 146:3,4 “Pumzi au Roho inapomrudia Mungu, mawazo hupotea”
1Timotheo 6:16 “Wanadam hawana uzima wa milele, ni Mungu pekee asiyepatikana na mauti”.
Rumi 2:7 “sisi tunatafuta uzima wa milele. Biblia inalitumia neno Roho mara 1600, lakini hakuna mahali inaposema roho isiyokufa”.
1Korintho 15:51-54 “Yesu atakaporudi ndipo tutakapovikwa kutokufa”.
Zaburi 115:17 “Wafu hawamsifu Mungu”.
Matendo 2:34 “Daudi hakupanda mbinguni alipokufa, bali anangojea kuja kwa Yesu na ufufuo wa kwanza”.
Muhubiri 9:5 “wafu hawajui neno lolote”.
Ezekiel 18:4Roho (Mtu) itendayo dhambi itakufa.
Ufunuo 1:17-18 “Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho na alie Hai, nami nalikuwa nimekufa natazama ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu. Yesu ana funguo za Mauti (Uwezo wa kuhuisha) kuzimu ni kaburini penye giza na sio motoni. Yesu ni limbuko la waliolala. Atawafufua wapendwa wetu waliolala siku atakaporudi mawinguni maana ana mamlaka. Alimtoa Lazaro aliyekufa siku nne. Paulo Mtume wa Kristo anaandika “Angalieni nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho. Maana parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilishwa. 1Wakorintho 15:51-52.
[5/7, 11:02 AM] +255 693 120 591: KIFO CHA MWANADAMU
MARA BAADA YA KIFO KUNA NINI ?
Kuna mafundisho mengi tofauti juu ya Mtu anapokufa, wengine wanasema anaenda kuzimu, wengine jehanamu, wengine peponi, wengine haendi kokote. Je Mungu anasemaje ?, jibu la kweli tunalipata kutoka katika Neno la Mungu kama lilivyochambuliwa kwenye vipengele vifuatavyo.
(1) MTU AU NAFSI HAI
Mtu au Nafsi HAI ni muungano wa vitu viwili MAVUMBI na PUMZI YA MUNGU, ( Mwanzo 2:7, Ezekiel 18:4 Isaya 53:12 ), Au NAFSI HAI = MAVUMBI + PUMZI YA MUNGU. Hivyo, vitu hivi viwili vikitengana hamna nafsi HAI na ndicho huitwa kifo, mtu anakuwa kuzimu.
(2) KUZIMU KUNA NINI ?
Maandiko yanasema KUZIMU ni sehemu penye ukimya, Mtu aliyekufa au aliyekuzimu hawi na Ufahamu, hivyo hajui lolote juu Mbinguni na Duniani. ( Mwanzo 3:19, Mhubiri 3:18-20, Mhubiri 9:5-6, Zaburi 104:29 ). Pumzi inayomrudia Mungu sio nafsi hai, hivyo inakuwa sawasawa tu na kabla ya mtu hajazaliwa au kuumbwa.
(3) WAKRISTO HALISI HUKIITA KIFO KUWA NI NINI ?
Neno la Mungu linasema kifo ni sawa na USINGIZI, Daudi alikiita kifo kuwa ni USINGIZI WA MAUTI. Kama mtu asivyojua lolote akiwa usingizini ndivyo Marehemu anavyokuwa kabulini hadi kristo atakapokuja. ( Daniel 12:2, Yohana 11:11, Mathayo 27:52, 1Thesalonike4:13, Ayubu 17:13, Luka 8:52-53, Zaburi 13:3, 1Korintho 15:20-23 ).
(4) KUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA WALIOKUFA NA MUNGU ?
Mungu hana uhusiano wowote na waliokufa, kwa sababu hawana kumbukumbu lolote, Pia Kristo alisema Mungu sio wa waliokufa. ( Mathayo22:32, Zaburi 146:1-4 ). Hivyo watakatifu wote waliokufa hawako Mbinguni wamelala kabulini.
(4) NI LINI WATAKATIFU WALIOKUFA WATAONANA NA MUNGU ?
Mbinguni au Peponi wanaenda watu hai au ( NAFSI HAI) wakivishwa miili ya Mbinguni ( Mfano: Eliya, Henoko, Kristo nk. ), Kristo kama alivyotuahidi atakuja kutuchukua pamoja na waliokufa atakapokuja mara ya pili. Tutarudishiwa Pumzi na kuwa hai tena, ndipo tutavishwa miili ya mbiguni na kuanza safari ya kwenda kwa Baba yetu Mbinguni. ( Yohana 5:28-29, 1Thesalonike 4:15-17, Yohana 14:1-3, 1Korintho 15:51-52, Ayubu 14:12, Matendo 24:15, Matendo 2:34 ). Yesu mwenyewe alipokufa msalabani na kuzikwa hakuenda mbinguni hadi alipofufuka ( Yohana 20:17 )
(5) LINI WAOVU WATAINGIA JEHANAMU ?
Waovu wataingia Jehanamu baada ya Kristo kupitisha hukumu, Ni ahadi ya kristo pia kuja siku ya mwisho kuuhukumu ulimwengu na kutoa adhabu ya Moto. Waovu watafufuliwa katika ufufuo wa pili, wote watakuwa hai na kudhihirishiwa matendo yao yote, ndipo MOTO utawashwa kwa ajili yao. ( Ufunuo 6:14-17, 20:13-15, 22:12, Mathayo 16:27, 2Petro3:7-10, Isaya 25:9, Yohana 5:28-29, Mathayo 25:31-41, Malaki 4:1, Rumi 2:5-6 ).
Viongozi wa dini wanaofundisha kuwa Mtu akifa hapohapo anaenda Jehanammu (Motoni) au Peponi (Mbinguni) ni lazima tuwaangalie sana huenda kwa kujua au kutokujua wanatumiwa na yule adui kwa hila kuvuruga ukweli halisi juu ya mpango wa Mungu Kuuhukumu ulimwengu kwa haki kama Injili inavyosema.
MAFUNGU YA BIBLIA YANAYOTUMIWA KUPOTOSHA UKWELI
WAEBRANIA 9:27.
Kama tulivyosoma hapo juu baada ya Kifo hakuna kinachoendelea, yaani mtu hana nafasi tena ya kuamua kufanya mema au mabaya. Kilichoandikwa kitabuni mbinguni dakika ya mwisho ya kukata Roho, ndicho kinapelekwa hukumuni siku ya mwisho Kristo atakapokuja. Mtu akifa rekodi za matendo yake zinafungwa tayari kwa hukumu. Pia neno la Mungu linasema hukumu kwa waliokufa imeshaanza, hii inaitwa hukumu ya upelelezi ambapo vitabu vya kumbukumbu kwa waliokufa vinapitiwa mmoja baada mwingine hadi siku ya Mwisho.
LUKA 23:39-43.
Hapa Kristo alikuwa anamhakikishia mhalifu kuwa watakuwa wote peponi, Neno halijasema "LEO HII" Kristo amesema "LEO HIVI". Hapo kuna makosa ya uchapaji na tafsiri kutoka lugha ya awali ya kigiriki, alama ya koma (,) kwa kiswahili sahihi haijawa mahali pake. Hata hivyo kama tulivyosoma Kristo alithibitisha kuwa hakuenda Mbinguni (Peponi) alipokufa ( Yohana 20:17, Yohana 14:1-3 ). Pia ukumbuke kuwa Mungu sio kigeugeu na neno lake halipingani.
LUKA 16:19-28.
Mfano huu wa Tajiri na Maskini Lazaro, umekuwa ni kigezo kikubwa cha Shetani kutumia kuwavuruga watu washindwe kuielewa Injili na ahadi za Kristo. Kabla ya kutoa maelezo juu ya mfano huo soma na kutafakari mifano mingine iliyotolewa na Kristo ( mfano: Luka 16:1-15 ) Je unaweza kusema "Kristo alihalalisha mali ya Udhalimu ? ", Mifano iliyotolewa kwenye Biblia, kabla hatujaichukuwa kama mafundisho, ni lazima tuangalie vitu vufuatavyo : Mfano ulitolewa na nani, Kwa watu wa aina au hali au Tabia gani, Dhumuni au Fundisho maalumu la mfano, na Je biblia nzima inasemaje juu ya Fundisho hilo.
Katika mfano huo Fundisho au Dhumuni lilikuwa juu ya hali halisi ya Matajiri wenye Ubinafsi na Maskini, itakavyokuwa wakati Kristo atakapokuwa akimlipa kila mtu mshahara wake. Kristo hakuwa na maana kuwa mtu akifa anakwenda Peponi au Jehanamu halafu wanakuwa wanawasiliana. Shetani anajua kuchanganya ukweli na uongo lakini kwa kuichambua biblia nzima kwa msaada wa Roho mtakatifu, siri zote za muovu zinafichuliwa. Watu wengi leo wamechanganyikiwa hadi wanasema biblia inajipinga.
MAFANIKIO YA SHETANI KUPITIA SOMO ZIMA LA WAFU
[A]
Shetani amefanikiwa kueneza uongo wake aliousema kwa mama yetu EVA katika Bustani ya Edeni. Mungu alisema "hakika mtakufa", Shetani alisema "hakika hamtakufa". Hata hivyo Mungu kwa njia ya manabii, Kristo na Mitume amezidi kuthibitisha kuwa Binadamu sharti afe, Kufa ni Amri tangia Edeni. Na shetani anaendeleze uongo kuwa Mtu hafi ila anabadilishwa mwili na kuwa na nafsi hai.
[B]
Amewaingiza wengi kwenye Ibada za Umizimu bila kujua. Kuomba, Kuongea na Wafu na kuwaombea wafu ni Ibada za Umizimu, Kwa kuamini kuwa Wafu wako mbinguni, Shetani anajigeuza na kuja kwa sura za watakatifu waliokufa na kuwaagiza watu wamwabudu Mungu kwa njia ambazo zingine ni kinyume na Maandiko. Ibada ya Sanamu, Lozari na sadaka ya wafu walioko pagatori ni baadhi ya mafundisho yaliyoingizwa kanisani kwa hila ya mwovu na wengi hawajui. Kuomba au kuwaombea Wafu Ni machukizo kwa Bwana ( Kumbukumbu la torati 18:9-12 ).
[C]
Amefanikiwa kueneza Imani ya Pagatori, ambayo amewafanya mamilioni ya watu wapotee, kwa kutojiandaa wakiwa Hai, wakitegemea kuja Kuombewa na kutolewa sadaka ya msamaha na ndugu zao walio hai ili watoke Pagatori na kwenda peponi.
[D]
Amewafanya wengi wachanganyikiwe wasielewe sawasawa Ahadi za Kristo juu ya Kurudi mara ya pili kuja kuuhukumu ulimwengu, na Injili kuhusu Kiama imevurugwa. Pia amewaminisha wengi kuwa Mungu si wa HAKI kwani anawapeleka Jehanamu kabla ya, Hukumu na wenye Mapesa wanaweza kumlipa wakasamehewa wakiwa pagatori, hivyo kumfanya Mungu kuwa anaupendeleo.
Ndugu yangu inakupasa uchague leo kuwa katika wokovu wa kweli au wokovu ambao Kristo aliuita wa watu
wapumbavu, yaani wale wanaomkiri Kristo kuwa mwokozi wao kwa midomo tu ila wanakataa kutii Neno lake.
Yesu anakuita kwa Upole na kukutahadharisha, Fanya uamuzi sasa.
[ Mathayo 7:24-27 , Ufunuo 18:4-5 ]
[5/7, 11:14 AM] +255 693 120 591: Kifo
Tuna na paswa kufanya nini wakati mauti yako machoni mwetu? Ikiwa mungu yu pamoja nasi tusiwe na hofu imeandikwa Zaburi 23:4 "Naam nijapopita kati ya ponde lauvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami gongo lako na fimbo yako vyanifariji."
Kifo kinafanana vipi? Nikama usingizi. imeandikwa 1Wathesalonike 4:13 "Lakini ndugu hatutaki msijue habari za waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini." pia Yohana 11:11-14 "Iliyasema hayo kisha baada ya hayo akawaambia, rafiki yetu Lazaro, amelala lakini nitakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia Bwana ikiwa amelala tapona lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake nao walidhani yakuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi Lazaro amekufa."
Danieli amesema nini kuhusu kifo? Imeandikwa Danieli 12:2 "Tena wengi wahao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka wengine wapate uzima wa milele wengine aibu na kudharauliwa milele."
Je? walio kufa wanajua lolote? Imeandikwa Mhubiri 9:5-6, 10Kwa sababu walio hai wanjua ya kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahauliwa mapenzi yao namachukio yao na husuda yao imepotea yote pamoja wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua, lolote mkono wako utakapolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri wala maarifa wala hekima huko kuzimu uwendako wewe."
Kifo sio mwisho! Imeandikwa Isaya 26:19 "Wafu wako wataishi maiti zako zitafufuka amkeni kaimbe ninyi mnao kaa mavumbini kwa maana umande wako nikama umande wa mimea nayo ardhi itawatoa waliokufa."
Yesu ametuhaidi nini kuhusu kifo? imeandikwa Hosea 13:14 "Nitawakomboa na nguvu za kaburi nitawaokoa na mauti ewe mauti yawapi mapigo yako? Ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafishwa na macho yangu."
Ufufuwaji uko katika nguvu za mungu imeandikwa 1Wakorintho 15:21-22 "Maana ya kuwa mauti ili letwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu italetwa na mtu kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadhalika na katika kristo wate wanahuishwa."
Mungu alimpa mwanawe kwa sababu gani? imeandikwa Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenada ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ila kila amwaminiye asipotee bali awena uzima wamilele."
Watu wema na wabaya watafufuliwa siku ya kiama imeandikwa Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote walio makaburini wataisikia sauti yake nao watatoka wao waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu".
Waaminifu watafufuliwa yesu akirudi mara ya pili imeandikwa 1Wathesalonike 4:16-18 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbiguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya mungu nao walio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo."
Tutafanana vipi baada ya ufufuo? Imeandikwa Wafilipi 3:20-21 "Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni kutoka huko tunamtazamia mwokozi Bwana wetu yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na mwili wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo uweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake."
Watakatifu wataishi mdagani? imeandikwa Luka 20:36 "Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo."
Wenye dhambi wta ngoja kwa mda gani kabla ya kiama? imeandikwa Ufunuo 20:4-5, 9 "Kisha nikaona vitu vya enzi wakaketi juu yake nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya uchuhuda wa Yesu... Hao walio wafu salia hawakuwa hai hataitimie ile miaka elfu,... 9 Moto ukachika toka juu mbiguni ukawateketeza."
Wenye dhambi ni nani? imeandikwa Ufunuo 21:8 "Bali waoga, wasioamini, wachukizao, wauwaji, wazinzi, wachawi, waabuduo sanamu, na waongo sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, hiyo ndiyo mauti ya pili."


No comments:
Post a Comment