» » Vanessa Mdee adai kuna msanii mkongwe anamchafua

Vanessa Mdee ameshindwa kuyavumilia yanayomtoka kinywani mmoja kati ya vigogo anaowaheshimu kwenye sanaa ya muziki nchini, hali iliyomsukuma kuanika ya moyoni.

Vee Money ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz ametumia mtandao wa Twitter kuyatoa ya moyoni dhidi ya kigogo huyo, ingawa hakuweka wazi jina lake.

“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” inasomeka tweet ya kwanza ya Vee Money.

Hata hivyo, mwimbaji huyo ameamua kuweka heshima yake mbele na kujiepusha na majibishano kwani kufanya hivyo anaamini kutakuwa utovu wa nidhamu.

Mwaka huu umeendelea kuwa mwaka wa mafanikio ya kupanda zaidi katika ngazi za kimataifa kwa Vee Money, ingawa amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutajwa kwenye orodha ya wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Msanii huyo ameendelea kukubalika ndani na nje ya nchi ambapo amekuwa akipewa mashavu kadhaa kung’arisha nyimbo za wasanii wa nchi za Afrika Kusini na Afrika Magharibi.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles