» » Korea Kaskazini: Tutafanya majaribio ya makombora kila wiki

Korea Kaskazini: Tutafanya majaribio ya makombora kila wiki

Korea Kaskazini ilifanya paredi kubwa siku ya JumamosiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini ilifanya paredi kubwa siku ya Jumamosi
Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake, Afisa wa juu nchini humo ameiambia BBC mjini Pyongyang, ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.
''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka," alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.
Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.
Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.
Bwana Han ameiambia BBC: ''Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...