» » SOMA KISAHIKI UTAJIFUNZA KITUG

  Kijana mmoja aliwaaga wazazi wake kwa ajili ya  kuianza safari yake ya kuelekea Mjini kwa ajili ya shughuli za kikazi.Wazazi wake hawakumkatalia kutokana na kwamba wao walikuwa wakimtegemea sana huyo Kijana wao wa pekee hivyo walimbariki na kumtakia safari njema huko aendako na walimuombea kwa Mungu amtangulie safarini .Maandalizi aliyafanya haraka haraka kutokana na kwamba wito wa kuelekea huko ulimjia kwa ghafla sana na kumtaka afike mapema iwezekanavyo. Aliandaa vitu vyake vyote vya mhimu na jioni ya siku hiyo akaelekea vituo vya mabasi kwa ajili ya kukata tiketi ya moja kwa moja ili asipate usumbufu njiani.Basi zoezi hilo alilifanikisha na kurudi nyumbani kumalizia maandalizi mengine madogo madogo.

  Kesho yake asubuhi na mapema Wazazi wake ambao walikuwa wamezeeka sana walijikongoja wakamsindikiza hadi stend za mabasi kuanza kusubiria basi alilokata tiketi lifike na yeye apande na kuondoka moja kwa moja.Baada ya dakika kumi basi lilifika na Kabla Kijana hajapanda Wazazi wake walimkumbatia huku machozi yakiwatoka,,Kijana aliwaondoa wasiwasi na kuwaambia Mungu atamuongoza na atarudi salama. Basi akapanda ndani na kuitafuta siti aliyokuwa amepatiwa na kisha akakaa na kusubiria Basi hilo liondoke ,,kwa vile bado abiria walikuwa wakiendelea kupanda, gari hilo lilikuwa limetulia.Wakati abiria wakiendelea kupanda ,ghafla aliingia kichaa mmoja akanyosha kidole chake kumwelekea yule Kijana na kumwambia.

"We kichaa shuka chini....we kichaa shuka chinii ". Kijana huyo hakumsikiliza huyo kichaa bali aliendelea kumpotezea tu.Yule kichaa alipoona Kijana hamsikilizi kwa mwendo wa haraka haraka alimfuata yule Kijana na kumshika mkono na kuanza kujaribu kumvuta huku akimwambia .

" We kichaa shuka chini tafadhari.. Shuka chinii ".Kijana alikasirika sana na kutaka kumpiga yule kichaa lakini watu wakamshurutisha sana amsikilize maana walihisi amemdhurumu kitu au amemnyang'anya kitu chake mhimu. Sintofahamu ilitokea ndani ya Basi hilo na kelele ziliongezeka sana.Basi yule Kijana alishuka chini akiwa na ghadhabu kubwa mno.Alimuangalia yule kichaa kwa jicho la hasira sana,na kichaa alipoona hivyo alianza kumcheka sana huyo Kijana. Kisha akaanza kukimbia, Kijana naye kwa hasira aliyokuwa nayo alianza kumkimbiza mpaka umbali wa mita mia mbili na hamsini.Alipochoka aliona isiwe taabu kuendelea kukimbizana na kichaa asiyeeleweka,alirudi haraka hadi ilipokuwa Basi yake.Kwa bahati mbaya aliikuta imeshaondoka kitambo,, Kijana alijilaumu sana ni kwa nini alimsikiliza kichaa na amemdanganya.Alikipiga piga sana kichwa chake na akaona tayari kashakula hasara.Kwa huzuni ilimbidi tu atumie gari jingine maana hakuwa na namna,,kwa bahati nzuri alifanikiwa kuupata usafiri mwingine na kisha safari yake ikaanza.

Baada ya kukimbia umbali wa kama kilomita kumi mbele ghafla gari yao ilisimama Mara baada ya kuliona Basi moja limepinduka vibaya na kujikunja Kama karatasi huku watu wengi waliokuwa wamekufa wakibebwa na kuingizwa kwenye gari maalumu za hospitalini wakiwemo na majeruhi ambao walivunjika miguu na viungo mbali mbali vya mwili,, Kijana alilitambua hilo Basi kwamba ndilo lile alilokuwa amelipanda mwanzoni Kabla ya kichaa kuja kumwambia ashuke chini.Kwa huzuni huku machozi yakimdondoka aliangua kilio cha juu Sana asiamini macho yake kama amenusirika na kifo.

Kule alipokuwa anaenda alifika salama Lakini bado machozi yalikuwa yakimtoka,,alimshukuru sana MUNGU kwa kumwokoa na kisha kumuomba amsamehe kwa upumbavu alioufanya wa kumdharau yule kichaa na kuapa kutorudia tena.

====>Ndugu yangu uliyekwisha kukisoma kisa hiki tambua Mungu kwa watu anaowajali kamwe huwa haachi wapotee.Katika dhiki, taabu, mateso na hata ajari huwa anatumia njia yoyote ile kumsaidia mtu anayempenda .Hivyo anaweza akatumia kitu kidhaifu sana ili akuokoe hivyo usikidharau.

Kama una maoni ushauri piga 0769436440  what's app

Download Apps ya Hi ya GSN NEWS

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...