» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 13 Na 14

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/WatSap, Email@yusuphngahala@gmail.com.Fb.com/MwalimuYusuph Abel Ng'ahala.Instagram@mwalim_yuu.

SEHEMU YA KUMI NA TATU.
Tulipoishia Akamaliza na kuichomoa kisha akavaa kofia na kuondoka zake. Hakika nilizidiwa ujanja. Nilianza kuhisi mabadiliko ya mwili palepale. kwani nilihisi____Endelea... Nakauka damu. Nilijikuta napiga kelele za kuomba msaada akaingia Peris na kuniangalia. Nilikua tayari nimekauka mithili ya ukuni mkavu. Sauti ikaanza kukwama. Peri akatoka na kuja na daktari. Aliponiona tuu akamtuma nesi alete drip la damu haraka. Hata haikupimwa ni kundi gani kwani kufanya hivyo ilikua ni kupoteza mda. Akanitundikia drip kisha akanidunga sindano fulani. Sikujua nini kilijiri hadi pale niliposhtuka nikiwa na hali nzuri kiasi. Wakati nafumbua macho nilimwona Peris yuko pale na Anthony wakilia. Nilijitambua ya kua mimi ni mtu mwenye thamani sana. Peris alipoona nimefumbua macho alishindwa kuzuia hisia zake. Aliinama na kunibusu mdomoni mara kadhaa.

Anthony akafuta machozi. Niliumia sana kumwona Anthony analia kiukweli. Mtoto mdogo kama yule aliumia kwaajili yangu nlikua kama niliyepandikizwa gunia la hasira. Peris akatoka na kwenda kumwita daktari. Akaja na kuniangalia kisha akashauri nihamishiwe chumba cha siri. Baada ya kuhamishwa na siku kadhaa kupita hali yangu ilikua nzuri kabsa. Japo nilibaki na makovu ya kumwagiwa tindikali lakini sikujali hilo. Zilipita wiki kadhaa nikifanyishwa mazoezi pale hospitali. Baada ya kua vizuri kabsa nikaruhusiwa kutoka. Nilipotoka hatua yangu ya kwanza ilikua kufikia ofisi za gazeti lile lililonichafua. Nilipofika nilimfuata mhariri mkuu. Nikamwuliza juu ya zile habari wamezipata wapi? Nilikua nimefura kwa hasira nilimkunja haswaa. Wakati anaanza kuongea ghafla kuna mwenzake akamshika begani. Mara jamaa akaanguka na kufa palepale. Hali ile ilinitisha na kuamua kumkamata yule jamaa. Chaajabu wakati napambana naye alikua akitumia sana pete yake.

Nikagundua ile pete inakitu. Nikamtageti vizuri kisha nikamkamata ule mkono wenye pete. Alipoona kazidiwa nguvu akajigusa na ile pete naye akapoteza maisha. Niliivua ile pete na kuiangalia ilikua na kimwiba flani cha kukunja na kukunjua. Nilitoka na kurudi nyumbani. Nilimkuta Peris yuko na Anthony. Kwakua nilikua bado sijatulia nikaenda kituoni kuona kama wameshafika ofisi zile za magazeti ili kuchukua maiti zile mbili. Pia nilikua naenda kuangalia ile pete ina nini. Baada ya kumwona mtaalamu wa pale ofisini Akanambia ile ni sumu kali sana. Hua inatumika na Wavietnam kuwaua Wamarekani. Wao hupaka kwenye mishale hivyo ukipatwa na mshale ule unakufa papo hapo.

Sasa sumu ya Vietnam Tanzania inafanya nini? Nikatoka na kumfuata mkuu mkuu. Alinipa pole kisha akasema nisiwe na shaka tayari taarifa zile wamezikanusha. Nikamshukuru kisha akanambia sasa inabidi niongezewe kikosi ili kuifanya kazi kwa ufanisi. Akaniletea maafisa upelelezi wanne. Wote walikua wametoka Marekani kwenye kozi za kipelelezi. Wa kwanza alikua Onesmo, Wa pili alikua Upendo, Watatu alikua Mwita, na wa nne alikua Khajara. Hivyo tukawa watu sita ukimjumuisha na Peris. Tulifahamiana pale kisha tukakubaliana tuanze kazi siku inayofuata.

Peris hakuwepo ila nilipaswa kumfikishia taarifa. Basi baada ya pale nilichukua baadhi ya dokumenti na mafaili yanayohusu wale majambazi. Nikatoka nlipofika nyumbani nakumbuka ilikua mida ya saa 12 jioni. Nilimkuta Peris sebuleni akiangalia Tv. Anthony hakuwepo nadhani alikua kalala. Peris alikaa kimtego sana. Nilijua alikaa vile baada ya kusikia gari inaingia. Nikamsalimia Akainua mguu na kuweka juu kama amekunja nne. Kisha akaitikia salama za utokako. 

Nikajibu nzuri. Lakini macho yangu yalikua yakimtazama Peris na kugundua kua hakuvaa kitu zaid ya khanga. Hivyo wakati ameinua mguu nilipata kuona mbali sana kwani khanga ilikua imemwachia eneo kubwa. Tamaa ikanivaa. Hisisia zikanitawala. Mapenzi yakateka akili yangu. Sikujua nifanye nini. Basi Peris akasimama na kusema nikupokee.?

Mmmmh mmmmh Aaah eeeee Saaa saaa sawa tuu. Niliitikia kwa kujikanyaga. Akachukua "briefcase" na kuanza kuelekea kuviweka chumbani kwangu. Alitembea kwa maringo huku sehemu za nyuma zikiniacha mdomo wazi. Nikaamua kumfuata kwa nyuma. Alipofika akaweka juu ya kabati. Lakini wakati anatoa mkono kule juu khanga yake ikaanguka. Nikaona kifua chake kizuri, kilikua kimesimama kama mtoto aliyetoka kuvunja ungo.Kitovu chake kilinitamanisha Pale nilipomwangalia kiuononi Mungu wangu. Nikajikuta nameza mate. Wakati anainama kuokota khanga akili yangu ikahama kabisaa. Nikamfuata na kumshika mkono. Alijua ninachotaka akaonyesha ushirikiano hatimae amri ya sita ikavunjwa. Mimi na Peris tukawa Mtu na mpenzi wake.

Usiku ule ulikua usiku mzuri sana. Asubuhi tukaamka na kujiandaa kwenda kazini. Tulipofika kazi ziliendelea kama kawaida. Tulishauriana upelelezi wetu ufanyike kwa mda mrefu lengo ilikua kuwatia nguvuni wote. Mwezi wa kwanza ukapita kisha wa pili na zaidi wa tatu. Tulikua tunakaribia kukamilisha upelelezi. Kwa bahati mbaya Peris alikua tayari mjamzito hivyo ilibidi awe anashinda nyumbani. Nakumbuka siku ambayo tulipanga kwenda kukamilisha upelezi wetu na kuanza operation ya kukamata wote. Siku hiyo ilikua Ijumaa nilikua njiani naenda ofisi ya wizara ya Mawasiliano. Wakati nafika nikamwona mtu akiwa amevaa kiaskari kama mimi anatoka pale mlangoni.

Baada ya kumwangalia vizuri alikua ni yule mwanaharamu anayefanana na mimi. Nilipata hasira Zabroni Zabroni! Nikashuka haraka kwenye gari. Mara naye akaingia kwenye gari na wakatoweka. Nikaingia kule kwenye ofisi za mawasiliano. Wakati nasukuma mlango nilikutana na Dimbwi la damu. Nikahamaki na kurusha macho mbele ambapo sikuamini ninachokiona. Wafanyakazi wote kila mtu kwenye kompyuta yake. Walikua wamekatwa vichwa na kuachwa pale.

Mle ndani ilikua ni bahari ya damu. Nilikua nikitembea juu ya damu. Nikawa nashangaa sana hali ile ilikua inatisha sana. Nikasogea huku na huko na kuona kama kuna yeyote yuko hai. Hapakua na dalili yoyote ya mtu kua hai. Nikawa najaribu kuangaza macho lakini wapi? Hao pekee walipaswa kutupa ushahidi wa mwisho je tutaupata wapi? Zabroni alikua ni mjanja na mwerevu kupindukia. Bahati mbaya nilisahau kupiga simu kituoni. Ghafla nikasikia king'ora cha gari za polisi zikija. Kwa vyovyote vile mimi ndo nitakamatwa mle ndani. Kosa ni kua sikutoa taarifa hivyo watasema mimi ndiye muuaji wa watu wote wale. Nikiwa nimeduwaa. Mara polisi waliingia na kuniweka chini ya ulinzi. Nikafungwa pingu na kupakiwa kwenye difenda kupelekwa kituoni kujibu tuhuma za mauaji._______________________

__________________________________________________________________________________________________________________________________Wajua nini kilifuata??? Kama hujui kutana na mwalimu yuu sehemu ya 14 upate majibu. Nawapenda wote kwa lolote nichek0755683295, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb nivist inbox kwa jina Mwalimu Yusuph Ng'ahala. Instagram @mwalim_yuu. Chaoooooo.

Siku hizi mbili Kuna Mambo ya liingiliana samahani Sana wapenzi wa simlizi hii. Naomba tuunge mpaka

SEHEMU YA KUMI NA NNE.
Tulipoishia Nikiwa nimeduwaa. Mara polisi waliingia na kuniweka chini ya ulinzi. Nikafungwa pingu na kupakiwa kwenye difenda kupelekwa kituoni kujibu tuhuma za mauaji._____Endelea...Tulifika kituoni nikatolewa kisha nikafunguliwa zile pingu. Walifanya vile kama sehemu ya heshima kwangu kisha wakanambia nahitaji ofisini kwa mkuu. Nilipanda ngazi kuelekea huko na nilipofika nilimkuta mkuu kachukia kiasi. Kisha akaniuliza Afande Yuu unafanya nini? Kwanini kila siku wewe? Mbona unadhalilisha vazi lako hivi? Mbona unadhalilisha jeshi la polisi! Haya siku zote unasingiziwa leo umekutwa eneo la tukio. Enhe na leo tudanganye. Moyo uliniuma sana kwakweli nikashindwa cha kujibu zaidi ya kudondosha chozi la uchungu.

Bora ungeua ukiwa hujavaa sare za jeshi. Unaua na vazi la jeshi la polisi juu. Unaisaliti nchi? Unalisaliti jeshi? Kwanini Yuu? Kwanini? Tazama Jeshi lilikuamini, nchi ilikuamini. Afisa mpelelezi. Afisa wa jeshi la polisi unaua hadharani ndani ya Sare. Bunduki uliyopewa na serikali yako. Ulikula kiapo utatetea na kulinda taifa kwanini umegeuka Yuu kwaaaa............ Kabla hajamaliza kuongea nilipatwa na hasira nikamkunja na kumnyanyua juu toka alikokua hadi karibu yangu. Nikamwambia mkuu Siyo mimi kwanini mnanilazimisha? Mkuu aliingiwa na woga kiasi alivoona kwa mara ya kwanza nimemkunja. Mara wakaingia askari wawili walipoona mkuu yupo kwenye kibano. Walianza kunipiga mimi. Walinipiga mpaka nikamwachia. Nilikua nimelowana machozi ya hasira. Mara mkuu akasema hebu nipisheni niongee na Yuu. Wakatoka.

Kumbe baada ya kumbana alihisi kua kweli mimi sihusiki. Akaniuliza kwa upole ndipo na mimi nikamwelekeza Mwanzo mpaka mwisho. Alikua mwelewa sana baada ya kukabwa. Basi akaagiza zile tape zilizokua zikirekodi matukio ziletwe. Basi zilipofika likaitwa jopo la maaskari 26 wenye weledi mkubwa. Wakaanza kuangalia. Mtu yule alionekana kweli ni mimi. Lakini bahati nzuri ni makovu ya tindikali yeye alikua hana. Hicho pekee kilitumika kua kigezo kikubwa cha kututofautisha mimi nilikua na makovu usoni yaliyotokana na tindikali. Ikaonekana kweli ushiriki wangu haupo. Basi wakasema sina hatia lakini nikapewa mda wa kumkamata Yule mtu. Basi nikawashukuru nikamfuata mkuu wangu na kumwimba radhi kwa kumkaba kwasababu ya hasira.

Akasema yameisha ila nifuatilie swala lile kwa umakini. Kisha naye akasema atajumuika nasi. Kwani taaluma yake ni alisomea mambo ya kijasusi huko nje. Basi askari wenzangu wakaniomba radhi na kunipa moyo nisikate tamaa. Nilishukuru makovu yangu yaliniokoa. Kitu unachodhani si cha muhimu na kina kuharibia ipo siku kitakuokoa. Jifunze kupenda kila kitu chako hata kama kibaya. Basi mda ukasonga hatimaye mda wa kurudi nyumbani ukafika. Nilianza safari kurudi nyumbani nikiwa na gari langu. Baada ya kufika nilimkuta mke wangu akiwa amekaa nje. Akikua akinisubiri. Nilimkumbatia na kumbusu. Mara kuna ujumbe ukaingia kwenye simu yangu. Nikafungua na kuusoma nao ulisomeka hivi. "Tayari watatu. bado wanne? Mtumaji jina likatokeza Zabroni kama kawaida yake.

Nilijua tuu kuna tatizo nikachukua simu na kumpigia Khajara alikua hapatikani. Nikampigia mkuu wangu ndipo simu ikapokelewa ikasikika ikisema. Zabroni hapa unasaje. Nilishtuka sana nikajua tayari mkuu katembelewa. Nilipiga simu kituoni ili maafande kadhaa wakamwangalie nyumbani kwake. Haikua kazi ngumu baada ya mda wakanipigia simu na kusema familia nzima ya Mkuu wameuawa kikatili sana. Mke wake alitolewa matiti, na mkuu alikatwa sehemu za siri.

Watoto watatu wote walikatwa kichwa. Nilitoka nyumbani na kwenda kushuhudia. Nikiwa njiani nilikutanana na gari moja ambayo nilihisi ina watu si wa kawaida. Nikaanza kuifuata kwa nyuma. Ilisonga sana nadhani badae walishituka kama nawafu tilia wakaongeza mwendo. Nikaongeza pia. Lakini kwa bahati mbaya kuna Basi la abiria lilikua "linaovatake" mbele kulikua na gari hivyo akalazimika kuingia mbele yangu. Hali ile iliwapa mwanya wa kukimbia. Kwani "nilipoovatake" sikuwaona. Nikaamua kuendelea na safari yangu.

Baada ya kufika kwa bosi nilishuhudia Mke wa bosi akiwa na alama za visu mwili mzima. Alitapakaa damu. Bosi ndo ilikua kakatwa sehemu za siri. Watoto kukatwa vichwa. Mara nikapata wazo nimpitie Mwita twende ofisini ili tupange mambo fulani. Nilitoka na kwenda kwa Mwita wakati nafika tuu. Niliikuta ile gari ndo inaondoka eneo lile. Nikaipiga picha haraka. Kisha nikaingia ndani kwa Mwita bila hodi. Nilishajua kua kuna hatari. Na nikweli ilikua hatari. Kwani wakati na naingia nilikutana na mkono mlangoni. Ulikua ni mkono wa Mtu kabisa. Nilipoinua macho nikakuta Paja la mtu liko mezani. Nilimeza mate ya woga. Kisha Nikapepesa macho ndipo nikaona kichwa cha Mwita juu ya kabati. Moyo ulidunda paa! Kwani macho alikua katoa kama vile yu hai.

Nilijiuliza hivi huu ni ukatili wa namna gani. Kwanini wanajiachia kiasi hiki hadi kumkatakata mtu vipandevipande kweli? Tumefika wapi watanzania. Nikaitoa simu na kuwataarifu kituoni. Wakati nimekata simu mara simu yangu ikawa inaita. Alikua ni Peris nikapokea kisha nikamsikia akisema. Baby kuna gari imepaki hapa nyumbani mda mrefu sasa hakuna mtu anayeshuka wala kuongea. Nikamwuliza ikoje. Aliponipa maelezo nikajua tuu ni ya wale wapuuzi.

Akasema tangu imefika waliipaki na hakuna mtu aliyeshuka mpaka mda huo. Na tayari wamekaa zaidi ya nusu saa. Nilishtuka nikamwambia hebu mfiche kwanza Anthony Basi akasema sawa. Ila yuko nje kwahiyo akipita watamwona tuu. Nikamwambia basi toka nje kisha mtoweke hapo. Akajibu sawa nikamwambia lakini kua makini akajibu sawa. Lakini wakati nataka kukata simu mara kwenye simu nikasikia sauti ya mke wangu okilia kwa kelele za woga. Aaaaaaa! ______________________________

______________________________ ___________________________________________________________________________________________Nini kilijiri? tukutane sehemu ya 15. Kwa lolote nicall 0755683295,Instagram @mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala ,Email@yusuphngahala@gmail.com. Nawapenda woteeeeeee



Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...