
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,Email@
SEHEMU YA KUMI NA SITA.
Tulipoishia Akaikimbilia na kuiwasha. Chaajabu akawa haondoki. Nilizidi kumsogelea Mungu wangu alikuakua ni Zabroni Makweka nililijua hilo baada ya kumkaribia. Nikamlenga na bastola yangu kisha nikafyatua risasi_____Endelea..........
Kwakua kituo chetu kilikua kimeshapoteza wakuu wawili. Hivyo nikapandishwa na kua mkuu wa kituo kama sehemu ya kutambua juhudi zangu. Maisha yakasonga huku nikiwa ndiye mkuu wa kituo kijana sana hapa Tanzania. Nilianza kurudisha ari ya kupendwa na kukubalika. Nakumbuka kuna siku niliitwa ikulu ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupongezwa kwa kazi nzuri. Ilinitia moyo. Hali ilitulia kwa mda kiasi ilipita miezi kama mitano hivi bila kua na matukio ya kihalifu. Mimi nilikua nazidi kuichunguza kesi ya majambazi watatu yaani, Zabron makweka, Jarome Singano na Nurdini. Ile kesi ilikua ni ngumu kupita kiasi kwani ilionekana kuna vigogo wa serikali wako nyuma yao. Ilinibidi nijipange haswaa ili kuwakabili.
******************************
Maisha ya mimi na Peris yalikua mazuri huku Anthony tukiwa hatujui kama yu hai au alishauawa na majambazi. Tangu siku aliyokamatwa tulifuatilia ngome zote bila mafanikio. Hatimae tulikata tamaa na kumwachia Mungu. Muda wa kujifungua Peris ulifika na akajifungua salama tulipata mtoto wa kiume. Furaha iliongezeka na kuwa maradufu. Siku zikasonga sana hatimaye Peris naye akatakiwa kurudi kazini. Tulikua tumeshampata dada wa kazi kwahiyo haikusumbua sana. Kazi ziliendelea pale kituoni huku mimi nikiwa ndiye bosi sasa. Pamoja na kwamba nilikua bosi nilikua bado nafanya kazi ya upelelezi na kujiapiza kua kwa maumivu waliyosababisha kwangu wale majambazi. Basi lazima niue wote kwa mikono yangu. Kuna siku Ilikua saa 12:45 jioni Peris alikua na "Shift" ya usiku lakini kwakua ana mtoto ilibidi nimruhusu kwenda nyumbani. Kwa kawaida mimi nilikua naondoka ofisini saa tatu usiku kila siku.
Siku hiyo mara baada ya Peris kuondoka kuna nyumba moja nilielekezwa kua Zabron huitumia sana kama sehemu ya kupanga mashambulizi. Nakumbuka nilimweka mlinzi eneo lile kama atamwona mtu kuingia anipigie simu. Nilipokea simu mida ya saa moja kua kuna mwanamke mmoja kaingia mle akiwa na wanaume wanne. Nilibadili nguo na kuvaa za kiraia ili nisigundulike kirahisi.Nikachukua pikipiki na kuwahi eneo lile. Nilipokaribia pikipiki nikapaki mbali sana kisha nikasogea kwa miguu. Nilifika na kukuta geti limefungwa. Nikaamua kuruka ukuta na kuingia ndani. Sikutaka kuwavamia kwasababu sikujua wana silaha gani.
Ilinibidi kupita madirishani kuchungulia. Nilichungulia madirisha kadhaa bila mafanikio. Mara nikafikia dirisha moja hapo nikapata kuwaona na kuwasikia kwa mbali. Lakini kuna sauti ile ya kike nilikua naisikia kama naifahamu sana. Nilisogea na kupenyeza jicho kwa karibu. Nikabahatika kuwaona wachache kutokana na udogo wa tundu. Nilimwona Zabroni akiwa kifua wazi na mezani kulikua na kitu kama ramani. Nilipokua nasikia maongezi yao walikua wakipanga kufanya shambulio. Sikujua ni wapi lakini walikua wakisema tutaingilia hapa na kisha kutokea huku. Walinzi huwa hapa lazima wauawe ili tufanikiwe. Kisha nikasik ia yule mwanamke akisema mimi nitawatarifu kila kinachoendelea. Sasahivi nimerudi kazini hivyo shaka ondoeni.
Lakini pia msiwe mnaacha kuja kunivamia maramojamoja ili kuwapumbaza wajue hata mimi naandamwa. Yule kwasasa naishi nae najua kila anachopanga hivyo msijali nitakua nawapa pia taarifa. Maneno yale yalikua yakinitisha sana kwani ile sauti ilikua si ngeni sana masikioni mwangu. Lakini kila nilipojaribu kupenyeza jicho nimwone ni nani sikuweza. Mara mipango yao ilikamilika na kuanza kuondoka. Walipokua wakitoka mimi nikatoka na kuwahi nje ili nijifiche niwashuhudie vizuri.Niliruka ukuta na nilipotoka sehemu pekee ya kujificha ilikua juu ya mwembe ulikua nje ya ile nyumba.
Nikakwea haraka na kujificha juu. Hapa nikawa naona chini kwa kiasi. Niliwaona wale watu kwa mbali wakitoka. Lakini macho yalikua kama yananidanganya ninachokiona. Nilikua namwona mtu kama Peris akiwa na Zabroni na wale wanaume wengine wanne. Nilijipa moyo na kusema hawezi kua Peris yule. Nikatoa simu mfukoni na kuipiga simu ya Peris ikawa haipatikani. Nikaamua nitulie mpaka watoke kisha nione mbinu mbadala. Walizidi kusonga na kuja ikumbukwe ilikua ni usiku hivyo nilichokua nashuhudia nilikua nasaidiwa na mwanga wa taa za ile nyumba hivyo sikua naona vizuri. Nilitamani kuanzisha mashambulizi lakini wao walikua wengi sana na nilikua sehemu mbaya hivyo ningemalizwa kirahi sana. Nikajipa moyo na kusema wacha wapite mimi nikaandae vikosi.
Walisonga mpaka getini huku wakiwa hawana wasiwasi wowote. Niliwashuhudia wakifunga geti na kuwasha kitu fulani. Kwa uzoefu nilijua ile ni shoti ya umeme hivyo lile geti ukilishika baada ya wao kuondoka unapigwa shoti. Walipomaliza wakazidi kuja kule kwenye mti mara walipofika karibu. Katika harakati za kupenyeza macho na kutoa matawi ili niwaone. Bahati mbaya nikagusa vibaya maembe mawili yakadondoka chini. Walikua tayari chini ya ule mti wanapita hivyo yale maembe yaliwafanya wataharuki Kisha wakatoa wote bastora zao. Mara nikasikia_____________________
SEHEMU YA KUMI NA SABA.
Tulipoishia Katika harakati za kupenyeza macho na kutoa matawi ili niwaone. Bahati mbaya nikagusa vibaya maembe mawili yakadondoka chini. Walikua tayari chini ya ule mti wanapita hivyo yale maembe yaliwafanya wataharuki Kisha wakatoa wote bastora zao. Mara nikasikia____Enda nayo........ Mmoja wao akisema oya acheni woga wa "kisenge" ayo si maembe halafu mnatoa silaha za nini sasa? Mwingine akadakia maembe hayo hayajaiva yanaamgukaje peke yake? Yule mwanamke akadakia hapa hua kuna ndege wanalala huenda ndiyo walioangusha haya. Basi wote wakarudisha bastola viunoni mwao na kuendelea na safari yao. Moyo ulitulia kisha nikashusha pumzi kwa mbali na kuhisi nimeokoka kutoka kwenye mdomo wa mamba. Nikatuliza kichwa kisha nikaanza kushuka kwa tahadhari.
Nilipofika chini nikakimbilia haraka pikipiki kule nilikoiacha. Nilipoifikia nikapata wazo la kuwahi nyumbani kumwangalia Peris kama yupo au laa! Nilijisemea moyoni ikiwa hayupo na kazini aliondoka tangu saa 12 jioni hakika atakua ndiye yeye niliyemkuta kule. Niliwasha pikipiki na kutoka kwa kasi ya ajabu. Nilipita njia za mkato ili niwahi kufika. Baada kama ya nusu saa nilifika nyumbani na kushuka kwa fujo kwenye pikipiki. Nikasonga ndani na kuingia sebuleni bila hata hodi. Sebuleni hapakua na mtu hivyo nikaingia chumbani. Nilipigwa na butwaa kumwona Peris kalala na mtoto. Tena walikua wamelala fo fo fo!
Nikaanza kumwamsha Peris kwa kumtingisha. Alionekana aliyekua kalala usingizi sana. Nikamemwasha sana hatimaye akaamka. Na kupiga mwayo. Akajinyoosha na kutupa shuka huko kisha akaniuliza Vipi mume wangu za kazi. Lakini chaa ajabu nilichokiona ni kua Peris alikua kavaa nguo za kawada kutokea. Haikua kawaida yake kwani nadhani ningemkuta na nguo ya kulalia. Nikaitikia safi mke wangu mbona umelala na nguo za kutokea? Na umerudi hapa saa ngapi? Kuna mahali ulipitia? Aaah "no!" "I mean" kuna mahali umepitia kabla ya kuja huku? Mtoto Amekula? Aaah "sorry" Hujapi.......
. Akadakia kwa kusema we vipi mbona maswali mengi mpaka nashindwa nijibu lipi niache lipi khaa! Kwani umepatwa na nini? Mmmh Aaah samahani mke wangu.
Kwakweli hali ile ilikua kama imenichanganya. Nikajikuta namtundikia maswali yasiyo na kikomo. Baada ya kushusha pumzi na kutuliza akili nikaamua nimpotezee tuu. Nikamwambia vipi mke wangu ulifika salama. Akajibu ndiyo mume wangu. Nikamwambia sawa. Mara akasema mbona hujarudi na sare za kazi. Pia sijasikia kama muungurumo wa gari. Nimehisi umerudi na pikipiki. Nikajibu ndio kumbe umenisikia wakati narudi ee? Sare nimeamua kuacha nitavalia kazini leo kuna mahali nilienda ambako sikupaswa kuwa na sare. Kichwani mwangu likaja swali kama alikua anasikia wakati mi narudi na pikipiki alishindwaje kusikia wakati namwamsha? Je alijifanya kalala makusudi. kupoteza maboya Mmh! Mbona kama sielewi haya mambo.
Kuna wazo likaja ya kua nimwache nifanye uchunguzi kwanza. Nikaamua kupoteza kwa kuendeleza stori zingine kabisa.Aliamka na kuniandalia chakula nikala kisha tukaenda kulala. Asubuhi tuliamka na kujiandaa kwenda kazini. Shuhuli ziliendelea kama kawaida. Siku zikasonga huku mimi nikiwa bado naifuatilia ile kesi kwa siri kubwa. Kuna siku nikapigiwa simu na mtu na kunambia kuna taarifa zinaonyesha uwezekano wa kuvamiwa kwa benki ya CRDB tawi la mwananyamala. Alipokata simu nikawaandaa vijana kadhaa kwaajili ya kufanya doria eneo lile. Basi vijana wangu walifika na kuzingira benki yote. Benki ilikua ikiendelea kutoa huduma kama kawaida. Baada ya masaa manne nilipigiwa simu na kuambiwa kuna mauaji yametokea ndani ya beki ile na kuna watu zaidi ya ishirini wameuawa.
Nilitaharuki kiasi kisha nikampigia simu yule niliyemwambia aongoze doria pale. Alipopokea nikamwuliza vipi hali ya U salama eneo lile akajibu kwa kujiamini hali ni nzuri na ulinzi umeimarishwa. Nikamuamuru kuingia ndani ya benki mara moja. Baada ya mda akanipigia simu na kunambia kuna mauaji yametokea mule ndani tena ya kutisha.
Nilianza kwa kumfokea sasa ni nini mlikua mnafanya hapo? Akajibu mkuu hata mimi nashangaa hawa majambazi wamepita wapi. Aaaaah hasira zilinizidi nikaamua kukata simu na kuamuru askari kadhaa twende eneo la tukio. Basi baada ya kufika pale benki nilikuta askari wakiwa wamezingira benki. Nilishuka kwenye gari na kuingia ndani na kukuta watu wengi wameuawa kwa risasi za hatari sana. Nilihisi kichwa kinazidiwa kwa mawazo mara nikapigiwa simu na afisa mmoja wa ikulu. Nikaipokea na kusikia nahitajika ikulu ya raisi haraka sana. Nilijua tuu ya kua natakiwa huko kwasababu ya lile tukio. Nikawaamuru wale askari kufunga eneo lile na asirugusiwe mtu kufika eneo lile. Lakini haikua inasaidia sana kwani tayari wizi ulikua umeshatokea. Nilianza safari hya kuelekea ikulu nikiwa njiani kulikua nafoleni kiasi. Wakati nimesimama Alikuja mtu mmoja na kuinama kwenye dirisha langu.
Nilikua sijamwona nikai nua kichwa na kumwangalia. Kwakua kioo nilikua nimekishusha. Yule mtu alikuakaingiza sura ndani kiasi lakini zaidi alikua amenilengeshea bastola. Zaidi ilinitisha kwani hakua mtu mwingine bali ni yule adui yangu wa siku zote Zabroni Makweka. Nilihiona kama nisiye na akili kuacha kioo wazi. Lakini kwa joto la Dar es salaam ningefanya nini. Nikiwa nimepigwa na mshangao nikamsikia akisema. Ukijitingisha au kufanya chochote nakuua. Na ikumbukwe alishanitageti kwa bastola.
Sikua na ujanja wowote. Nikabaki nimeshikilia usukani wa gari. huku mate mdomoni yakiwa yanakauka. Kisha nikamsikia akisema. Mimi ndiye niliyekupigia simu. Nilitaka tukutame hapa. pia pole kwa niliyokusababishia pale benki ni ujuzi mdogo tuu umetumika. Zaidi akasema sasa kilichonileta ni hiki. Naomba simu zako zote. Naomba laptop yako na kama unakitafuta kifo kataa sihitaji kubishana. Huna nafasi ya kuongea.Nipe ninachotaka au nikuue hapahapa. Niliamua kutoa simu zangu laki laptop sikua nayo niliiacha ofisini. Basi akainuka mara nikasikia honi nyuma. Kumbe foleni ilishaanza kusogea. Nikamwona Zabroni akiondoka kwa kutembea na suti yake ya gharama haswaa. Nilijiona mjinga nisiye na akili ninayezidiwa na watoto wa mjini. Wakati naendesha gari mara nilihisi kama kitu nyuma ya gari. Nikageuka na kuona kuna__________________________
wambie watu wa dowblod apps ya 4sn news wawe wanapata kwenye simu zao
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment