Serikali imetangaza kuanzia June 2
hadi 4, 2017 Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama
nchini kote ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Tanzania ambayo
yatafanyika kitaifa Butiama mkoani Mara.
Waziri wa Mazingira na Muungano
January Makamba amesema tayari utaratibu umeshafuatwa ikiwa ni pamoja na
kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na TANAPA kuwa katika siku
hizo tatu Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama.
Maadhimisho ya siku ya mazingira
duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika June 5 mwaka huu Butiama Mkoani
Mara huku kukitarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa kuhusu
utunzaji wa mazingira.
Akizungumza na wanahabari jana,
waziri wa wizara hiyo, January Makamba alisema lengo la kupeleka
maadhimisho hayo Butiama ni kumuenzi Nyerere ambaye alikuwa mwanamazingira
namba moja nchini sanjari na kukumbuka mchango wake katika masuala ya uhifadhi
wa mazingira nchini.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment