» » Rais wa Korea Kusini ahoji mfumo wa ulinzi wa Marekani

Rais mpya wa Korea Kaskazini Moon Jae-in ameapishwa rasmi

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais mpya wa Korea Kaskazini Moon Jae-in ameapishwa rasmi
Rais mpya wa Korea Kusini, Bwana Moon Jae-In, ameanza kazi rasmi afisini kwake baada ya kuapishwa.
Bwana Moon ametoa wito kupunguza uhasama kati ya Korea Kusini na Kaskazini na wakati huohuo kutaka kujua ni kwa nini Marekani iliweka makombora ya Ulinzi katika ardhi ya nchi yake.
Amesema kuwa angependelea kutembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Wakili huyo wa haki za kibinaadamu anayejulikana kwa maoni yake huria anataka kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini kinyume na sera iliopo kwa sasa.
Pia ameapa kuliunganisha taifa hilo linalokabiliwa na ufisadi ambao ulisababisha mtangulizi wake kushtakiwa mbali na kuimarisjha uchumi.
Bwana Moon aliapishwa kuwa rais wa 19 wa Korea Kusini na kujaza pengo lililowachwa wazi na Park Geun hye.
Mwanachama huyo wa chgama cha Democrat amejionyesha kuwa mtu ambaye anaweza kuliendesha mbele taifa hilo kutoka kwa ufisadi mbali na kuliunganisha.
Mfumo wa kujilinda na makombora uliowekwa na Marekani nchini Korea Kusini
Image captionMfumo wa kujilinda na makombora uliowekwa na Marekani nchini Korea Kusini
Pia amekosoa mamlaka ya hapo awali kwa kushindwa kuzuia utengenezaji wa silaha wa Norea Kaskazini na ameapa kuimarisha uchumi na kuangazia tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana ambalo ndio tatizo kubwa la wapiga kura.
Uongozi wa bwana Moon utaangaliwa huku kukiwa na wasiwasi mwingi katika eneo hilo.
Marekani na Korea Ksakazini zimekabiliana kimaneno katika majuma ya hivi karibuni baada ya Pyongyang kufanya majaribio ya makombora

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...