» » Ndege za China zazuia ndege ya Marekani


Haki miliki ya pichaAFPImage captionNdege za China zaizuia ndege ya Marekani

Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani.

Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China.

Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.

China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.

China yarejesha chombo cha MarekaniChina: Marekani itatue mgogoro wake na Korea KaskaziniChina na Marekani waitisha suluhisho la amani Korea kaskazini

''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema.

''Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea.

Image captionBahari hiyo ya kusini mwa China

Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.

Ndege na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.

China yataka Marekani na Korea Kaskazini kuvumilianaChina yaionya Marekani kuhusu visiwa vinavyozozaniwaChina yakamata chombo cha Marekani baharini

Kwa nini bahari hiyo ya kusini mwa China inazozaniwa?

Mnamo mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.

Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles