» » Nalaumu FBI na wadukuzi wa Urusi BI. Clinton

Hillary Clinton amelilamu shirika la FBI na wadukuzi wa Urusi kwa kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu

Image captionHillary Clinton amelilamu shirika la FBI na wadukuzi wa Urusi kwa kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton amewalaumu wadukuzi wa Urusi na mkurugenzi wa Ujasusi nchini humo kwa kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu uliopita
Aliambia mkutano mjini New York kwamba angeshinda kura hiyo iwapo uchaguzi huo ungefanyika tarehe 20 mwezi Oktoba kabla ya kuchapishwa kwa barua ya mkurugenzi wa FBI James Comey akilielezea bunge la seneti kwamba FBI imeanzisha uchunguzi kuhusu hatua yake ya kutumia barua pepe za binafsi.
Alisema kwamba alikuwa amefanya kampeni nzuri na akapoteza kutoka na maswala yaliofanyika katika kipindi cha siku kumi za mwisho.
Anasema kuwa sasa amerudia uanaharakati akisema hatua yake inalenga kuweka upinzani mkali dhidi ya rais Trump ambaye amemkosoa kwa sera zake za kigeni mbali na utumizi wake wa mtandao wa Twitter.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles