» » MWENYEKITI CCM Ashangaa Kutajwa Kwenye Orodha ya Wenye Vyeti Feki Wakati Hakusoma



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Chamwino, Charles Ulanga ameshangazwa baada ya kutajwa miongoni mwa watu wenye vyeti feki cha kidato cha nne na kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya sekondari.Sakata la Mwenyekiti huyo ni mwendelezo wa utata ulioibuka baada ya ripoti ya matokeo ya uhakiki huo uliobaini wafanyakazi 9,932 wa Serikali na Taasisi zake kuwa na vyeti vya kughushi, kutumia vya watu wengine au cheti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja.Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, amesema wakati wa uhakiki alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu ‘A’.“Nawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?” amehoji Ulanga.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles