» » Mabibi harusi wakabidhiwa silaha ya kujilinda India

Mamia ya mabibi harusi katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.

Haki miliki ya pichaAP
Image captionMamia ya mabibi harusi katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.
Mamia ya mabibi harusi katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.
Ujumbe kama ''tumia dhidi ya mlevi'' umeandikwa katika ubao huo ulio na urefu wa sentimita 40 na hutumika sana kundoa uchafu katika nguo.
Gopal Bhargava , waziri wa maswala ya ndani nchini humo alisema kuwa anataka kuangazia swala la unyanyasaji wa wanawake waliopo katika ndoa.
Aliwaambia kujaribu kuafikiana na wanaume zao kabla ya kutumia ubao huo unaojulikana kama Mogri na hutumika sana kuondoa uchafu katika nguo,'' fanyeni mazungumzo mwanzo'',alisema.
Bwana Bhargava alichapisha picha za mabibi harusi waliobeba mbao hizo katika ukurasa wake wa facebook.
Aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba amekuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya wanawake wa mashambani ambao hunyanyaswa na wanaume walevi
''Wanawake wanasema kwamba kila wanaume wao wanapokunywa na kulewa chakari wanawapiga''.
''Fedha walizohifadhi huchukuliwa na kutumiwa kununua pombe'', alisema.
''Hakuna dhamira ya kuwachochea wanawake kufanya ghasia lakini ubao huu ni wa kujilinda dhidi ya ghasia''.
Mabibi harusi hupewa ubao ili kujilinda dhidi ya unyanyasaji unaofanywa na wanaume zaoHaki miliki ya pichaHINDUSTAN TIMES
Image captionMabibi harusi hupewa ubao ili kujilinda dhidi ya unyanyasaji unaofanywa na wanaume zao
Bwana Bhargava anayetoka katika chama cha Janata Party cha waziri mkuu wa India Narendra Mody anasema kuwa ameagiza mbao 10,000 kwa jumla.
Takriban mabibi harusi 700 walipokea mbao hizo katika harusi ya halaiki nyumbani kwake huko Garhakota wikendi iliopita.
Harusi za halaki hufanywa ili kuwasaidia watu wenye mapato ya chini kufunga ndoa bila kulipia hafla hiyo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa ilikuwa njia ya kupata uungwaji mkono kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...