» » Hivi ndivyo ilikuwa maporomoko ya mawe yalivyo funga barabara Tanga


Jeshi la Polisi mkoani Tanga jana  lilifunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba  alisema, maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini

"Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..

"Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict

Kwa upande mwingine Kamishna huyo alisema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri.


Download Apps ya 4sn news

WhatsApp 0769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...