Waziri mkuu nchini DRC ajiuzulu
Haki miliki ya pichaGOOGLEImage captionSamy Badibanga
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Samy Badibanga amejiuzulu kama sehemu ya makubaliano yaliyoongozwa na kanisa katoliki kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo, kwa mujibu wa Redio moja ya nchi hiyo, Redio Okapi.
Hii inafuatia hotuba ya hapo jana kutoka na Rais Joseph Kabila, ambapo aliwaambia wabunge kuwa atamteua waziri mkuu kutoka upinzani ndani ya saa 48 zinazokuja.
Bwana Kabila alisema kuwa atafuata tararibu zilizoafikiwa kama sehemu ya makubaliano na upinzani ambayo yanataka uchaguzi kuandaliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki duniaMwana wa Tshisekedi kuongoza upinzani DRCWatu 17 wafa wakihofia kuvamiwa na waasi DRC
Kumekuwa na msukosuko nchini DRC baada ya Kabila kukataa kundoka madarakani wakati muhula wake ulipokamilika mwezi Disemba.
Mshirikishe mwenzako

No comments:
Post a Comment