» » Wanamgambo wa ETA wanasambaratika Ulaya

Wanamgambo wa ETA wanasambaratika Ulaya

Wanamgambo wa ETAHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanamgambo wa ETA
Kundi linalotaka kujitenga huko Basque ETA limethibitisha rasmi taarifa kuwa linapanga kusalimisha silaha Jumamosi tarehe 8. BBC imepata taarifa inayosema kuwa kundi hilo litasalimisha silaha zote na milipuko kupitia wawakilishi wa mashirika ya kijamii.
Punde tu mpango huo utakapo kamilika, hatua hiyo itamaliza ghasia za miongo kadhaa zilizosababisha vifo vya wau zaidi ya 800 na kujeruhiwa kwa maelfu wengine katika kampeni kali ya kundi la ETA katika kupigania uhuru wa Basque katika maeneo ya Uhispania na Ufaransa.
Na iwapo ETA itasalimisha silaha zake itakuwa ndio mwisho wa uasi Ulaya. Kundi hilo linatarajiwa kuvunjika katika miezi inayokuja.
Barua ya ETA
Image captionTaarifa ya ETA inasema wanamgambo hao watawasilisha silaha kupitia wawakilishi wa mashirika ya kijamii
Kwa miongo kadhaa, kundi la ETA lilihusishwana milipuko, mauaji na uporaji. Kwa wafuasi wake ilikuwa ni kupigani uhuru wa Basque, kwa waathiriwa wa ghasia zake, umekuwa muda wa uoga mwingi na kupoteza wapendwa.
Leo eneo la Basque huko Uhispania ni tofuati. Hakujashuhudiwa mashambulio kwamiaka kadhaa na ETA lilitangaza hatua ya kusalimisha silaha mnamo mwaka 2011. Lakini imechukua wakati wote huu kuwashawishi wafuasi wake kufanya hivyo, na kujaribu kusaka silaha zilizosalia.
Taarifa ya ETA hatahivyo inaonya kuwa wale inaowataja kuwa maadui wa amani huenda wakaizuia hatua yao. Lakini duru zilizohusika katika mpango huu zinasema kuna matumaini mpango utatekelezwa katikanamna ambayo itaridhisha na kukubaliwa na pande zote ikiwemo serikali ya Uhispania ambayo daima imekataa kujadiliana na ETA.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...