» » Rais Magufuli atapokea taarifa vyeti feki LEO

Rais Magufuli atapokea taarifa vyeti feki LEO

RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais katika Ikulu Ndogo ya Chamwino Dodoma, Jaffar Haniu ilisema taarifa hiyo itawasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba, 2016. 

Hivi karibuni wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Magufuli alisema anasubiri ripoti kuhusu watumishi wa umma wenye vyeti feki wapatao 9000.

“…Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisisitiza Rais katika hotuba yake hiyo.



A

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...