» » Muungano wa Tanzania leo wafikisha miaka 53

Muungano wa Tanzania leo wafikisha miaka 53

TanzaniaHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha Muungano huo.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan , ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Aidha,Amesema hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa kwamba unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.
Kuhusu elimu ya Muungano kwa Vijana, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande zote Mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.
Amesema kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...