» » Mlipuko wa bomu wawaua zaidi ya watu 100 Syria

Mlipuko wa bomu wawaua zaidi ya watu 100 Syria

Moshi uliotanda baada ya mlipukoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoshi uliotanda baada ya mlipuko
Gari lililokuwa limejaa mabomu likiendeshwa na mtu wa kujitolea mhanga limegongeshwa kwenye basi lililokuwa likiwahamisha raia wa Syria kutoka mji mmoja unaoshambuliwa.
Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu kadhaa waliokuwa kwenye basi hilo wamefariki hasa katika maeneo ya Aleppo na kwamba vipande vya miili yao vimeonekana kutapakaa kila mahali.
Waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini AlepoHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWaliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini Alepo
Wachunguzi wa mambo yanayoendelea Syria wanasema kuwa zaidi ya watu 100 walifariki.
Msafara huo wa mabasi ulikuwa ukiwabeba wakaazi wa eneo hilo na wapiganaji wanaounga Serikali mkono kutoka vijiji viwili vya Washia chini ya mpango wa mapatano kati ya Serikali na waasi.
BBC map
Image captionSyria
Wahamaji walichelewa kusafirisha kutokana na sintofahamu juu ya idadi ya waasi wanaopaswa kuruhusiwa kuondoka kutoka vijiji hivyo.
Licha ya mashambulizi hayo, ubadilishanaji wa raia na wapiganaji umerejelewa huku mabasi yakiingia katika maeneo yanayothibitiwa na Serikali na yale ya waasi.
Watu walikuwa wakisubiri kuabiri magari wakati mlipuko ulitokeaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu walikuwa wakisubiri kuabiri magari wakati mlipuko ulitokea

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...