» » Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana za kijeshi

Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana za kijeshi

Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana za kijeshi
Korea Kaskazini imejaribu kufyatua kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa kombora hilo lililipuka sekunde chache baada ya kufyatuliwa katika ufuo wa Mashariki wa Korea Kaskazini.
Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.
Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.
Hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani imekuwa ikipanda, huku kila upande ukijigamba jinsi utakavyoweza kuchafua upande mwingine.
Mnamo Ijumaa Uchina iliitisha mkutano unaonuia kutuliza uhasama huo.
Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshi

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles