» » MASOMO YA VIJANA SEHEM YA PILI CHAGUA MAISHA SEHEMU YA PILI

mwendelezo wa somo:
Sehemu ya pili

KUSOMAPAMOJANENO LAMUNGU Soma  Danieli  1:1-21 1) Kwa  nini  Danieli  na  rafiki  zake  watatu  walichaguliwa  kupata  elimu  hiyo? 2) Wakati  Danieli  na  rafiki  zake  walipochukuliwa  mateka,  unafikiri  walikuwa  wanafikiria mambo  gani  juu  ya  maisha  yao  ya  usoni?    Unafikiri  walipenda  kuondoka  nyumbani  na kuishi  katika  jumba  la  mfalme? 3) Danieli  alichagua  kufanya  nini  katika  kipindi  hiki  cha  mafunzo?    Mungu  aliuheshimu uchaguo  wa  Danieli  na  kumtuuza  na  nini? 4) Kama  vile  Daniel  na  rafiki  zake  walivyokabiliwa  na  mvuto  wa  mila,  vijana  wengi  siku hizi wanakabiliwa na mvuto wa mila na jamii kutenda mambo yaliyo kinyume.  Baadhi ya  mivuto  kama  hiyo  ni  ipi? 5) Fikiria  juu  ya  uchaguo  ambao  Danieli  na  rafiki  zake  waliufanya.    Unajifunza  mambo gani  kutoka  katika  hadithi  hii  ambayo  unaweza  kuitumia  katika  maisha  yako? MAMBO YAKUFIKIRIAPAMOJA Kufanya  Maamuzi  ya  Busara Kama  vijana  hao  wanne  katika  hadithi  ya  kwanza,  pengine  nawe  pia  una  ndoto  mbali mbali  juu  ya  maisha  yako  ya  usoni.    Unaweza  kuwa  na  ndoto  ya  kuendelea  na  masomo hadi  Chuo  Kikuu  mara  utakapomaliza  masomo  yako  ya  shule  ya  upili.    Unaweza  kuwa unafikiri  juu  ya  kusafiri  katika  nchi  mbali  mbali.    Unaweza  kuwa  na  fikira  za  kuishi  nyumbani  na  kuwa  mkulima.    Pengine  unafikiria  juu  ya  mke  utakayemwoa  au  mme atakayekuoa  au  vile  familia  yako  itakavyokuwa. Je! Unaweza kutimiza ndoto zako?  Wakati mwingine mambo kadhaa yaliyo juu ya uwezo wako  yanaweza  kukuzuia  usitimize  ndoto  zako.    Mara  nyingi,  ni  mambo  yale  unayoyachagua  kila  siku  yanayoamua  ikiwa  utatimiza  ndoto  zako  au  la. Rafiki ni watu muhimu katika maisha yako.   Rafiki unaowachagua ndio watakaokushawishi  kutenda  na  kusema  na  vile  uwezavyo  kuutumia  wakati  wako.    Mambo  unayoyatenda au  kuyasema  ndiyo  yatakayowafanya  watu  wengine  unaoishi  nao  wakuheshimu  au wakudharau.  Vile unavyoutumia muda wako kuyafanikisha masomo yako ama kazi zako nyumbani.    Iwapo  utafanikiwa  shuleni  unaweza  kuendelea  na  masomo  yako  hata  kuwa  na kazi  itakayokupatia  mshahara  mzuri  zaidi  kuliko  wale  ambao  hawakuendelea  na  masomo. Iwapo  utafanya  kazi  kwa  bidii  shambani  utaheshimiwa  na  wengine  katika  familia  yenu  na jumuia  yenu.    Unaweza  kuwa  hata  kiongozi  katika  jumuia  yako. Uchaguzi  mmoja  mbaya  unaweza  kubadilisha  mambo  kabisa.    Ukichagua  kuibia  mtihani utafukuzwa  shuleni.
Ukichagua  kufanya  mapenzi  kabla  ya  ndoa  unaweza  kupata  UKIMWI  kitu  ambacho  kitakufanya  usiishi  muda  mrefu  hadi  pale  utakapowaona  watoto  au  wajukuu  wako. Kufanya  uchaguzi  si  kitu  rahisi  sana  kama  vile  ambavyo  mtu  anaweza  kufikiria.    Wakati mwingine  inaonekana  kana  kwamba  kuna  mambo  mengi  ya  kuchagua;  wakati  mwingine kuona  kwamba  hakuna  uchaguo  mzuri  hata  kidogo.    Ni  mambo  gani  yanayoweza  kukusaidia  kufanya  uchaguo  utakaokusadia  utimize  ndoto  zako? Hizi  ni  hatua  ambazo  zinaweza  kukusaidia  kuamua 1. Orodhesha  mambo  unayopenda  kuchagua Chukua  muda  kuandika  mambo  kadhaa  unayoweza  kuamua  kulingana  na  uamuzi wako  utakavyokuwa  katika  miaka  kadhaa  ya  usoni.    Kwa  mfano,  rafiki  yako  ameamua kwenda  jijini  kutafuta  kazi  na  akataka  aende  pamoja  nawe.    Mambo  gani  yaweza kukukabili  katika  kufanya  uamuzi  huo?    Moja  ni  kukubali  kwenda  pamoja  na  rafiki yako  na  lingine  ni  kubaki  nyumbani. 1.  Fikiria  juu  ya  matokeo  mazuri  ama  mabaya  ya  kila  jambo. Andika  matokeo  mazuri  ama  mabaya  katika  kila  uchaguzi  ulioandika  hapo  juu.    Kwa mara  nyingine  tena,  yaandike  mambo  hayo  ili  uweze  kulinganisha  kwa  urahisi.    Je! Kutakuwa  na  matokeo  gani  ukienda  mjini?    Unaweza  kupata  kazi  na  kujipatia  fedha. Unaweza  kuendelea  kuishi  na  rafiki  yako  atakayekusaidia.    Je!  Kuna  madhara  gani yatakayokupata?    Utatengana  na  familia  yako.    Yawezekana  usipate  kazi.    Utahangaika kupata  chakula.   3. Jaribu  kufahamu  neno  la  Mungu  linavyosema  juu  ya  uamuzi  wako Neno  la  Mungu  linatupatia  mwongozo  wa  kila  hali  inayotukabili.    Katika  hadithi  ya Danieli na rafiki zake tunaona hawakufanya kitu rahisi, lakini pia walifanya kitu sahihi. Mungu  aliubariki  uchaguo  wao  mgumu  walioufanya.    Kutokana  na  mfano  huo,  uchaguo  sahihi  kwako  ni  upi? 4. Tafuta  ushauri  wa  busara! Chukua  muda  kuzungumza  na  watu  mbali  mbali  wanaokufahamu  vizuri  na unaowathamini  kama  vile  wazazi,  shangazi  au  mjomba,  mchungaji,  au  rafiki  yako mzuri  juu  ya  mambo  mbali  mbali  unayoweza  kuchagua.      Kubali  wakuulize  maswali kulingana  na  uamuzi  wako.    Wanaweza  kuwa  na  mawazo  mengine  ambayo  hukuwa umeyafikiria.   5.  Omba Kumbuka  kuwa  hakuna  uamuzi  ulio  mdogo  hata  usiweze  kuuombea  mbele  za  Mungu (Wafilipi  4:6-7).    Usisumbuke  iwapo  hutapata  majibu  kulingana  na  vile  ulivyofikiri  au kulingana  na  vile  wengine  wanavyofanya.    Endelea  kuleta  maswali  yako  mbele  za Mungu  naye  atakuwa  mwaminifu  kukujibu  kwa  njia  zake  ambao  huwezi  kutarajia  kwa  kubadilisha  mambo  fulani  katika  maisha,  kwa  kuubadilisha  mtazamo  wako  ama kwa  kuwatumia  watu  wengine  katika  maisha  yako.    Wakati  mwingine  jibu  laweza  kuwa "hapana"  ama  "subiri." Ahadi  ya  Mungu  juu  ya  maisha  yako Ni  jambo  la  kupendeza  kuendela  kuishi.    Kuna  mambo  mengi  ya  kuchagua  ambayo yasingeweza  kufikiriwa  na  watu  wa  zamani,  lakini  pia  kuna  changamoto  za  maisha ambazo  watu  wa  zamani  hawakukabiliana  nazo  -  kuenea  kwa  virusi  vya  HIV  na  UKIMWI, kuvunjika  kwa  ndoa.    Pengine  huwezi  kuhangaishwa  na  vyakula  vinavyotia  unajisi  kama vile  Danieli  alivyofanya.    Hata  hivyo,  kama  vile  Danieli  na  rafiki  zake  watatu,  utakabiliwa na  maamuzi  juu  ya  kuutunza  mwili  wako  usitiwe  unajisi.    Unaweza  kumtumaini  Mungu kwa  ajili  ya  maisha  yako  ya  usoni  kwa  kutii  amri  zake  na  kusubiri  baraka  zake  katika maisha  yako.    Ama  unaweza  kuamua  kufanya  kama  vile  upendavyo.    Jipe  moyo  kwa  vile katikati  ya  maamuzi  haya,  ahadi  za  Mungu  ni  za  kweli  kama  vile  zilivyokuwa  katika  siku zile  za  Danieli  na  rafiki  zake. Fikiria  ahadi  hizi  zifuatazo • "Kwa  maana  nayajua  mawazo  ninayowawazia  ninyi,  asema  BWANA,  ni  mawazo  ya amani,  wala  si  ya  mabaya,  kuwapa  ninyi  tumaini  siku  zenu  za  mwisho."  (Jeremia  29:11) • "Mambo  ambayo  jicho  halikuyaona  wala  sikio  halikuyasikia,  wala  hayakuingia  katika moyo  wa  mwanadamu,  mambo  ambayo  Mungu  aliwaandalia  wampendao."  (1 Wakorintho  2:9) • "Kwa  maana  mimi,  BWANA,  Mungu  wako,  nitakushika  mkono  wako  wa  kuume, nikikuambia,  Usiogope;  mimi  nitakusaidia."  (Isaya  41:13) • Yesu  alisema,  "…Mimi  nalikuja  ili  wawe  na  uzima,  kisha  wawe  nao  tele."  (Yohana  10:10) KUTUMIANENO LAMUNGU KATIKAMAISHAYAKO 1. Chukua  ahadi  moja  kutoka  katika  orodha  ya  ahadi  iliyo  hapo  juu  na  uikariri  ili  uwe tayari  kuikumbuka  wakati  utakapotakiwa  kufanya  uamuzi  fulani  katika  maisha  yako. 2. Chukua  muda  kuandika  baadhi  ya  ndoto  ulizo  nazo.    Fikiri  juu  ya  maamuzi  fulani ambayo  unaweza  kuyafanya  katika  siku  za  usoni  ili  uweze  kutimiza  ndoto  zako.    Omba na  kukabidhi  ndoto  hizo  mbele  za  Bwana,  mwombe  akuongoze  kufanya  maamuzi  ya busara.
Itaendelea Juma nne

kama una ushauri maoni Habari tupigie au tuma ujumbe whatsapp 0769436440

download apps ya 4sn news usipitwe na vitu vizuri mda wote tuko na wewe kukuletea kilicho bora 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles