» » Marekani yakatiza ufadhili kwa UNFPA linalohusika na mpango wa uzazi

Marekani yakatiza ufadhili kwa UNFPA linalohusika na mpango wa uzazi

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionUNFPA huhimiza afya ya uzazi na mpango wa uzazi katika takriban nchi 150 duniani

Marekani imesitisha ufadhili kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu, UNFPA unaotoa msaada kwa ajili ya mpango wa uzazi kote duniani.

Hatua hiyo italifanya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kupoteza takriban dola milioni thelathini za ufadhili kwa mwaka huu pekee.

UNFPA limepinga madai kuwa linafadhilili shughuli za uaviaji mimba.

Trump kuteua jaji anayepinga uavyaji mimbaUavyaji mimba: Wachangisha fedha kupinga sheria ya TrumpTrump hayuko juu ya sheria, jaji asema

Hili ni shirika la kwanza la Umoja wa mataifa kukabiliwa na kupunguwa kwa ufadhili baada ya ahadi ya kupunguza msaada wa kifedha kutoka kwa utawala wa Trump.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBalozi wa Marekani kwa Umoja wa mataifa Nikki Haley anasimamia uwezekano wa kupunguza ufadhili kwa Umoja huo

Hii ina maana kuwa UNFPA litapoteza ufadhili wa siku zijazo zikiwemo dola milioni 32.5 zilizokuwa zimepangwa kutumiwa mwaka huu.

Wizara ya mambo ya nje Marekani inasema kuwa uamuzi huo ulizingatia shughuli za UNFPA za mpango wake wa uzazi na serikali ya Uchina, ambazo inasema ulisaidia kuavya mimba na kufunga uzazi kwa lzima.

Sheria ya kupiga marufuku punyeto bungeni MarekaniTrump hajui apeleke wapi mshahara wakeWatakaoumia na watakaofaidi chini ya Trump Marekani

Badala yake ufadhili huo utaelekezwa katika mipango mingine ya uzazi katika nchi zinazoendelea.

Shirika hilo hatahivyo limesema kuwa madai hayo ''si sahihi'', na kwamba kazi zake zote zimekuwa ni za kuboresha haki za kibinfasi na wanandoa kuchukua maamuzi yao bila ubaguzi.

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles