» » Makonda: Nina Imani Roma na Wenzake Watapatikana Kabla ya Jumapili Hii

Makonda: Nina Imani Roma na Wenzake Watapatikana Kabla ya Jumapili Hii

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.

Alisema hayo jana akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.

Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi.

“Natoa pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunahangaika kujua wapi waliko. Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda.

Alisema tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao watakuwa wamepatikana.

==>Msikilize hapo chini akiongea

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles