» » Jumuiya ya kimataifa yalaani shambulio linaloshukiwa kuwa la gesi ya kemikali nchini Syria

Jumuiya ya kimataifa yalaani shambulio linaloshukiwa kuwa la gesi ya kemikali nchini Syria


watotoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatoto wengi kutajwa kuathirika zaidi
Jumuiya ya kimataifa imelaani shambulio linaloshukiwa kuwa la gesi ya kemikali dhidi ya mji unaodhibitiwa na waasi nchini Syria, shambulio linaloripotiwa kuua watu takriban 58.
Shirika la kimataifa linalopambana na matumizi ya silaha za kemikali OPCW limesema linakusanya ushahidi.
Naye mkuu wa sera za mambo ya nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amesema pande zote na wadau kwenye vita ya Syria wanatakiwa kupata suluhu ya kisiasa
SyriaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZahati ni miongoni mwa sehemu zililengwa katika shambulio hilo
Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano kuhusu mustakabali wa Syria, Mogherini amesema EU inategemea kila mmoja kutimiza wajibu wake kumaliza vitendo vya umwagaji damu.
''sisi Umoja wa Ulaya, si tunaotekeleza mashambulizi, sisi si tunaopigana, sisi ndio tunaotoa misaada ya kibinaadam, kuusaidia Umoja wa mataifa kufikia makubaliano na suluhu ya kisiasa na sisi ndio tunaokuwa tayari kuwasaidia raia wa Syria kujenga mustakabali wao kwa ajili ya taifa lao, hii ndio njia tunayotumia, hii ndio namna tunavyoamini sera ya nje inavyopaswa kutekelezwa, na tunasisitiza hilo, lakini haimaanishi kuwa mtu aharibu kila kitu kisha tulipe gharama. hili kamwe haliwezi kutokea'' alieleza
Kufuatia shambulio la anga jimboni Idlib kulitolewa ripoti zikisema kuwa mamia ya watu hasa watoto walikuwa wakitapika, kupaliwa na kutoja povu mdomoni
Serikali ya Marekani imesema shambulio lililotekelezwa Syria ni la kukemewa. Msemaji wa Serikali Sean Spicer ameinyooshea kidole serikali ya Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuhusika na mashambulizi hayo.
Syria imekana kutumia silaha za kemikali.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura siku ya Jumatano kujadili shambulizi hilo
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles