» » Afrika Kusini yapata waziri mpya wa fedha

Afrika Kusini yapata waziri mpya wa fedha


Malusi GigabHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMalusi Gigab
Waziri wa Fedha mpya wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba, amesema wakati umefika wa kubadilisha sana uchumi.
Amesema, kwa muda mrefu Afrika Kusini inahodhiwa na wawekezaji wa nchi za nje.
Pia amekiri kwamba kutolewa kazini kwa waziri aliyemtangulia hapo jana, Pravin Gordhan, kumeigawa nchi.
Bwana Gordhan anayeheshimiwa kimataifa, alipotolewa kazini ghafla, katika mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyofanya Rais Jacob Zuma, kulizuka malalamiko kutoka kwa watu wengi, pamoja na makamu wa rais, Cyril Ramaphosa, na wanasiasa mashuhuri katika chama tawala cha ANC.
Vyama vya upinzani, vinasema, Bwana Gordhan aliondolewa, kwa sababu alimzuwia Rais Zuma na washirika wake, wasipate nafasi ya kufikia mali ya taifa.
Bwana Gordhan alifutwa hali iliyozua kushuka kwa masoko ya hisaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBwana Gordhan alifutwa hali iliyozua kushuka kwa masoko ya hisa
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles