Wagombea wakuu wafanya kampeni za mwisho Uholanzi
Image captionWaziri mkuu Mark Rutte (kushoto) na mpinzani wake mkuu Geert Wilders (kulia) katika mdahalo
Viongozi kutoka vyama vikuu vya siasa watakao simama katika uchaguzi mkuu wa jumatano nchini Uholanzi wanafanya kampeni zao za mwisho kwa njia ya televisheni.
Wanajaribu kutafuta kura za mwisho za wale ambao pengine hawakuwa tiyari kupiga kura.
Vyama vyenye upinzani mkubwa ni kile cha mrengo wa kulia cha waziri mkuu wa sasa Mark Rutte na kinachopinga kuwepo ndani ya umoja wa ulaya na pia kupinga wahamiaji cha Geert Wilders.
Mwandishi wa BBC wa eneo hilo anasema kuwa uchaguzi huo unachukuliwa kama kipimo iwapo vyama vyenye sera kama za bwana Wilders bado vina ushawishi Ulaya.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment