Upasuaji wa kupunguza unene wa mwanamke mwenye kilo 500 wafanyika India
Mwanamke wa Misri anayeaminiwa kuwa mwenye uzito wa juu zaidi duniani akiwa na kilo 500, amefanyiwa upasuaji wa kupunguza unene chini India.
Msemaji wa hospitali ya Saifee mjini Mumbai amesema kuwa Eman Ahmed Abd El Aty, mwenye umri wa miaka 36, amepungua kilo 100 baada ya upasuaji.
" Tunajaribu kumuwezesha kuwa mwenye nguvu za mwili kuweza kusafiri nyumbani Misri haraka iwezekanavyo," ilieleza taarifa ya hospitali.
Familia yake ilisema kuwa hajawahi kuondoka nyumbani kwao kwa miaka 25 hadi siku aliposafirishwa hadi India mwezi Januari kwa ndege.
- Mwanamke mzito zaidi duniani apelekwa India
- India: Ujumbe wa dhihaka wamsaidia polisi kutibiwa
- Mwanamke "afufuka" India
Msemaji wa hospitali ya Saifee ameiambia BBC kuwa anaweza kupungua kilo za mwili zaidi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.
Upasuaji huo ulifanywa na kundi la madaktai walioongozwa na daktari bingwa wa upasuaji wa kupunguzunene wa mwili, Dkt. Muffazal Lakdawala.
Upasuaji wa kupunguza uzito na unene wa mwili unaofahamika kama -Bariatric surgery, kwa lugha ya kitaalam hutumiwa kama suluhu la mwisho kumtibu mtu ambaye ana uzito unaohatarisha maisha yake.
Familia ya Bi Abd El Aty' wanasema kuwa alikuwa na kilo 5 wakati alipozaliwa na alipatikana na ugonjwa wa matende, unaosababisha sehemu za mwili kuvimba kutokana na maambukizi ya wadudu aina ya kupe.
Wakati alipofikia umri wa miaka 11, uzito wake ulikuwa umeongezeka haraka na akapata kiharusi, hali iliyomfanya kuishi kitandani.
kwa sasa anahudumiwa ma mama pamoja na dada yake.
Hata hivyo Dkt. Lakdawala aliiambia BBC mwezi Disemba kwamba anaamini Bi Abd El Aty hana ugonjwa wa matende bali anaumwa unene wa kupindukia unaosababishwa na kuvimba kwa miguu.
Upasuaji wa bariatric unafanyika vipi
Bariatric surgery, ambao pia unafahamika kama upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili, hufanyika kama suluhu la mwisho la tiba ya mtu mwenye unene wa kupindukia na mwenye kiwango kikubwa cha mafuta mwilini.
Aina mbili zinazofanyika mara kwa mara za upasuajiwa kupunguza uzito wa mwilini ni:
- Gastric band, upasuaji ambao hufanyika kuzuwia ukubwa wa tumbo ili kiasi kidogo cha chakula kiweze kumshibisha mtu
- Gastric bypass, huu ni upasuaji ambapo mfumo wa kusaga chakula hubadilishwa na kuufanya kupokea chakula kidogo tu cha kusaga na hivyo chakula kidogo ndicho huruhusiwa kusagwa ili kumfanya mtu kuhisi ameshiba.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment