» » TTB yaitangaza Tanzania eneo bora la utalii duniani

TTB yaitangaza Tanzania eneo bora la utalii duniani

Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imejipanga kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii katika maonyesho ya Kimataifa ya Utalii yajulikanayo kama Internationalle Tourismus Borse (ITB) yaliyoanza rasmi jijini Berlin Ujerumani katika eneo la Messe Berlin na kuhudhuriwa na jumla ya nchi 187 kutoka kote duniani.

Mratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo ambaye pia ni Meneja Masoko wa Bodi ya TTB, Geofrey Meena amesema TTB imejipanga vilivyo kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani ambapo pamoja na kuendelea kuvitangaza vivutio v kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, Hifadhi  za Taifa, fukwe na maeneo mbalimbali ya kihistoria.

Pia mwaka huu mkazo umewekwa katika kutangaza ushahidi wa nyayo za binadamu wa kale (Zamadamu) uliovumbuliwa miaka milioni nne iliyopita katika eneo la Laetoli lililoko takribani kilometa 45 kusini mwa Olduvai Gorge.

“Pamoja na kuvumbuliwa kwa fuvu la anayesadikiwa kuwa ni binadamu wa kwanza kabisa duniani huko Olduvai Gorge Ngorongoro, lakini katika kuendelea kudhihirisha kuwa Binadamu wa kwanza aliishi Tanzania tumeamua katika maonesho ya mwaka huu kuja na ushahidi unaoelezea ukweli huo kwamba Binadamu asili yake ni Tanzania,” amesema Meena

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...