Trump na Merkel watofautiana kuhusu uhamiaji
Image captionTrump na Angela Merkel wa Ujerumani
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na chansela wa Ujerumani Angela Merkel katika kikao cha kwanza cha ana kwa ana kwa majadiliano lakini imebainika wazi katika mkutano na waandishi habari kwamba wametofautiana kuhusu maswala ya uhamiaji, uhusiano wao na Urusi na hata biashara ya kimataifa ambapo Donald Trump alidai Marekani imekuwa ikipunjwa katika mikataba ya kibiashara iliyoweka saini.
Amesema sera ambayo amekuwa akiinadi si ya kujitenga bali ni kuelezea kwamba Marekani imekuwa ikionewa na hivyo kutafuta usawa wa haki katika biashara
Kwa upande wake Bi Merkel amehimiza faida za kuendeleza biashara huru ya kimataifa.
Trump atangaza sera zake kuhusu UhamiajiTrump akumbana na wakati mgumu kupinga uhamiajiUhamiaji Marekani: Mameya wampinga Donald Trump
Pia ametoa wito wakimbizi watendewe haki kwa kuwa na uwazi katika kushughulikia maswala yao.
Japo viongozi hao wawili walijitahidi, ni dhahiri bado kuna ukakasi katika uhusiano wao kutokana na jinsi Trump alivyomsema bi Merkel vibaya katika hotuba zake za wakati wa kampeni.
Mshirikishe mwenzako

No comments:
Post a Comment