Rais wa Korea Kusini aondoka ikulu baada ya kutimuliwa madarakani
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionPark Geun-hye
Rais wa Korea Kusini aliyetimuliwa mamlakani Park Geun-hye, ameondoka rasmi katika Ikulu ya Rais mjini Seuol, baada ya mahakama ya nchi hiyo kumvua wadhfa wa urais kutokana na kashfa ya kupotea kwa mabilioni ya pesa chini ya utawala wake.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMsafara mkubwa ulimsafirisha kuenda nyumbani kwake katika wilaya ya Samseong.
Bi Park sasa amepoteza kabisa uwezo wa kutofunguliwa mashtaka ambao marais huwa nayo, na huenda akakabiliwa na mashtaka ya ubathirifu wa pesa, baada ya kumkubalia rafiki wake kuhusika katika kashfa kubwa ya kupotea kwa pesa ili kupendelewa kisiasa.
Mahakama yamng'atua mamlakani rais wa Korea KusiniWabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea KusiniKorea Kaskazini yasema inajiandaa kushambulia Japan
Bi Park alindoka ikuli ambayo inafahamika kama Blue House leo Jumapili, baada ya kuwapa kwaheri wahudumu wake.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionWafanyakazi walionekana wakiingiza bidhaa za Park ndani ya nyumba yake
Msafara mkubwa ulimsafirisha kuenda nyumbani kwake katika wilaya ya Samseong.
Mamia ya wafuasi wake walikuwa wakimsubiri huko huku karibu polisi 1000 wakitumwa.
Hwang Kyo-ahn, ambaye ni mtiifu kwa Bi Park sasa ndiye kaimu Rais.
Haki miliki ya pichaAPImage captionMaandamano ya kumpinga Park
Tume ya uchaguzi nchini humo inasema kuwa uchaguzi ulio huru na wa haki utafanyika ifikapo tarehe 9 mwezi Mei.
Maelfu ya watu walimiminika barabarani mjini Seoul siku ya Jumamosi kusherehekea kuondoka kwa Bi Park, huku umati mkubwa wa wafuasi wake nao ukikusanyika eneo tofauti.
Mshirikishe
No comments:
Post a Comment