» » Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania

Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania

Haki miliki ya pichaMALAWI AIRLINES / FACEBOOKImage captionNdege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda na Lusekelo Mwenifumbo

Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limetangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake pekee Alhamisi wiki hii.

Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.

Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .

Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya AirbusTanzania kununua ndege mpya ya BoeingTanzania yanunua ndege zake mbili

Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.

Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Haki miliki ya pichaMALAWI AIRLINES / FACEBOOKImage captionShirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo

"Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines ilisema.

Ndege ndefu zaidi hatimaye yapaa Uingereza

Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.

Mada zinazohusiana

MalawiTanzaniaWanawake

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...