» » Nay wa Mitego akamatwa na polisi Morogoro..... ni kutokana na wimbo wake unaoikosoa serikali

Nay wa Mitego akamatwa na polisi Morogoro..... ni kutokana na wimbo wake unaoikosoa serikali

Mwanamuziki  Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi leo asubuhi mkoani Morogoro na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero mkoani humo.

Nay wa Mitego amekamatwa akiwa hotelini Morogoro baada ya kuamaliza shughuli zake zilizompeleka ambapo alitakiwa kuongozana na polisi hao hadi kituo cha polisi.

“Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote. ✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo.” Ameandika Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Licha ya kuwa mwanamuziki huyo hajaeleza sababu ya kukamatwa kwake, au Jeshi la Polisi kutoa taarifa, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni wimbo wake alioutoa siku za hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo.

Wimbo huo umezungumzia mambo mengi hasa ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa sasa ikiwa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uhuru wa vyombo vya habari na  masuala ya sanaa.


T picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...