» » Benin yajadili rais kuongoza kwa muhula mmoja

Benin yajadili rais kuongoza kwa muhula mmoja

Haki miliki ya pichaAFPImage captionRais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.

Bunge nchini Benin limekuwa likifanya mjadala kuhusu marekebisho ya katiba ikiwemo kupunguza muda wa rais kuongoza hadi muhula mmoja wa miaka sita.

Kwa sasa rais anaweza kuongoza kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.

Lakini pendekezo hilo linakabiliwa na utata.

Merkel kuwania muhula wa nneNkurunziza aashiria kuwania muhula wa nne BurundiAli Bongo aapishwa kwa muhula wa pili

Vuguvugu moja la upinzani lilifanya mgomo mbele ya bunge likisema kuwa raia wanafaa kupewa fursa ya kujadili mabadiliko hayo.

Nchini Benin marekebisho ya kikatiba yanaweza kuidhinishwa kupitia kura ya maoni ama wingi wa kura bungeni.

Bunge la Gambia laongeza muhula wa JammehRais wa Zambia aapishwa kwa muhula mwingine

Rais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles