» » Mahakama yamng'atua mamlakani rais wa Korea Kusini

Mahakama yamng'atua mamlakani rais wa Korea Kusini

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais wa Korea kusini aliyengatuliwa mamlakani na mahakama Park Guen Hye

Mahakama ya juu nchini Korea Kusini imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye mamlakani.

Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.

Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.

Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.

Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.

Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.

Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.

Rais wa Korea Kusini tayari kujiuzuluWabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea KusiniRais wa Korea Kusini alinunua dawa za Viagra

Rais huyo sasa amepokonywa uwezo wa kutoshtakiwa na sasa anaweza kusimamishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWapinzani wa Park Geun Hye walisherehekea uamuzi huo katika barabra za mji wa Seoul

Bi Park alikuwa amesimamishwa kuhudumu kama rais tangu mwezi Disemba huku waziri mkuu wa taifa hilo akichukua majukumu ya kuongoza taifa.

Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.

Bi Park ameshtumiwa kwa kushirikiana na Choi.

Maelfu waandamana wakimtaka rais wa Korea Kusini ajiuzuluMaandamano ya kumpinga rais wa Korea Kusini yafanyika Seoul

Jopo la majaji wanane katika mahakama ya kikatiba liliangazia mashtaka yanayomkabili bi Park na kuamua kwamba kulikuwa na sababu mwafaka za kumwachisha kazi.

Haki miliki ya pichaAPImage captionWafuasi wa rais huyo walibubujikwa na mchazo baada ya uamuzi huo.

Makundi ya watu yalikuwa yemekongamana nje ya jengo la mahakama hiyo kusikiza uamuzi utakaotolewa swala ambalo limezua maandamano katika mji mkuu wa Seoul na miji mingine.

Mahakama iliamuru kwamba alitoa nakala nyingi za siri ikiwa ni ukiukaji wa kiapo alichokula cha kulinda siri za serikali mbali na kukiuka sheria kwa kumruhusu bi Choi kuingilia maswala ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...