Mahakama: sheria ya mitandao ni sawa kikatiba Tanzania
Mahakama Kuu nchini Tanzania imeamua kwamba vifungu tata viwili vya sheria ya makosa ya kimtandao viko sawa kikatiba.
Hii inamaanisha kushindwa kwa kampuni ya Jamii Media ambayo ilikuwa mlalamikaji katika kesi hii ambayo ilifunguliwa March mwaka jana
Jamii Media ilifungua kesi ya kupinga kifungu cha 32 na 38 cha Sheria ya makosa ya kimitandao ambavyo pamoja na mambo mengine, vilikuwa vikiamuru utolewaji wa majina ya wachangiaji wa mitandao na kuwapa polisi mamlaka ya kupekua na kuzuia vifaa vya mawasiliano vya mtuhumiwa
Mwanasheria wa Jamii Media Benedict Alex amesema watakata rufaa dhidi ya hukumu hii.
Kwa upende wake mwanzilishi mwenza wa mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo, amesema hukumu hii ni tishio kwa uhuru wa kujieleza, katika mtandao na hata nje ya mtandao
"Kwa aina hii ya hukumu, naona jeshi la polisi likitumia vifungu hivi vya sheria vilivyo na mapungufu kulazimisha wamiliki wa mitandao kufichua majina wachangiaji wao, jambo ambalo linawaweka wafichua siri hatarini"
Jamii Forums ni mtandao unaotajwa kuwa chanzo cha kufichua kashfa kubwa za rushwa nchini Tanzania ambazo nyingi zilichukuliwa na kuendelezwa na vyombo vingine vikubwa vya habari nchini humo
Hata hivyo mwaka jana mwezi Desemba, jeshi la polisi nchini humo lilimkamata Melo na kumlazimisha afichue majina ya wachangiaje wa mtandao wa Jamii Forums
Tangu kupitishwa kwake mwaka 2015, sheria ya makosa ya kimtandao imekuwa ikikosolewa na wanaharakati wa uhuru wa habari na kujieleza na kushutumiwa kuwa ni sehemu ya mpango wa serikali kukandamiza uhuru wa kujieleza nchini Tanzania
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment