Maelezo kwa picha: Teknolojia ya mazingira ya picha na grafiki
Sio siku zote kuwa wapiga picha wanaweza kupata picha tunazohitaji kuielewa taarifa. Mwandishi wa habari wa BBC, Nick Higham anazungumza na Amanda Farnsworth, mhariri wa Kitengo cha Uandishi wa Vielelezo vya Picha, kutaka kujua vipi vielelezo vinasaidia kufanya taarifa ngumu ifahamike.
Siyo ripoti zote zitanufaika kwa grafiki, lakini zinaweza kufaa sana kwa zile ambazo zinahitaji kutumia taswira, kuwaza kitu fulani kimekaa vipi.
Kwa mfano, mitambo gani inatumika kukagua sakafu ya bahari kuu kutafuta viumbe visivyojulikana? Jee chombo cha kuchunguza Mars kinafanya kazi vipi? Na handaki la Benki Kuu ya UIngereza linalohifadhi vinoo vya dhahabu limekaaje? Kukiwa na muda, watengezaji maalumu wanaweza kuonesha yale yanayoelezewa na waandishi wa habari wa BBC.
Kuna njia mbili kuu za kutumia mazingira ya picha: njia ya kama “kumtosa” mtangazaji kwenye mazingira mepya, kama juu ya Mars, au kueleza taarifa inayotatiza kwa kutumia ramani na nambari.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment