Lewis Hamilton ana imani ya kumshinda Sebastian Vettel
Dereva wa magari ya Langalanga Muingereza Lewis Hamilton anasema ana uhakika atamshinda Sebastian Vettel katika mashindano ya dunia ya Australian Grand Prix.
Hamilton alimaliza wa pili kwa Mjerumani huyo wakati wa kuanza kwa msimu mjini Melbourne, kufuatia shinikizo la mwendo wa kasi wa dereva huyo wa Ferrari.
"Litakuwa shindano kali, nina imani kuwa tutawashinda," Hamilton alisema .
"Ni vizuri tutakuwa shindano hili kali"
"Kuna kazi kubwa mbeleni, tuna mengi ya kufanya lakini hata hivyo tuko na furaha," alisema Vettel.
Hamilton naye amesema kuwa anachotarajia ni ushindani ulio mkali na Vettel mwaka huu wote.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI




No comments:
Post a Comment