Kwa Picha: Ndege ya wanawake pekee kutoka Malawi yatua Tanzania
Image captionShirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo
Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.
Ndege hiyo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.
Ndege ndefu zaidi hatimaye yapaa Uingereza
Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam.
Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Image captionMarubani wa ndege hiyo
Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, ambaye alisomea urubani jijini Addis Ababa, Ethiopia amemwambia Munira Hussein wa BBC kwamba alihamasishwa kuwa rubani na baba yake ambaye pia alikuwa rubani.
Image captionNdege hiyo uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Image captionMwelekezi pekee wa ndege wa kike uwanja wa JNIA Fatuma Kahabi.
Mada zinazohusiana
Mshirikishe mwenzako

No comments:
Post a Comment