» » Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny afungwa jela siku 15

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny afungwa jela siku 15


Alexei Navalny (kushoto) aliitisha maandamano kupinga ufisadi ndani ya serikaliHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAlexei Navalny (kushoto) aliitisha maandamano kupinga ufisadi ndani ya serikali
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, amehukumiwa kifungo cha siku 15 jela kwa kukiuka amri za polisi wakati wa maandamano makubwaa siku ya Jumapili.
Bwana Navalny alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliokamatwa kwa kuhusika kwenye mikutano kadha kote nchini.
Mahakama mjini Moscow mapema ilimpiga faini ya karibu dola 350 kwa kupanga maandamano yaliyoharamishwa.
Leo Jumatatu, serikali ya Urusi iliulaumu upinzani kwa kuchochea kuvunjwa kwa sheria na uchokozi.
"Baadhi ya vijana walilipwa kushiriki maandamano," msemaji wa polisi alisema.
Baadhi ya waandamanaji walibeba bata au mabango ya bataHaki miliki ya pichaAP
Image captionBaadhi ya waandamanaji walibeba bata au mabango ya bata
Bwana Navalny baadaye alimshutumu tena Dmistry Medvedev kwa kuhusika kwenye ufisadi.
Bwana Navalny alifikishwa mahakamani ya kukamatwa siku ya Jumapili na kushinda korokoroni. Licha ya kukwepa kifungo kwenye mashtaka ya kwanza, alihukumi kifungo cha siku 15 jela kwa kumpuuza afisa wa polisi.
Wakili wa bwana Navalny Olga Mikhailova, aliliambia shirika la Reuters kuwa, aliitarajia hukumu kama hiyo na kuwa atakata rufaa.
Kabla ya hukumu kutolewa leo Jumatu, bwana Navalny mwenye umri wa miaka 40, aliandika kwenye mtandao wa akiwa mahakamani akisema , "Hello kila mmoja, ni kutoka mahakama ya Trerskoy. Wakati utawadia tutawaweka hukumuni."
Alidai kuwa bwana Medvede ndiye anastahili kushtakiwa kama mwandalizi mkuu wa maandamano, kwa sababu ya vitendo vyake vya ufisadi vilivyochangia watu kuingia mitaani katika miji 99 nchini Urusi.
Alexei Navalny alikamatwa JumapiliHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAlexei Navalny alikamatwa Jumapili
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...